Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha MT. Agustino cha Tanzania (SAUT) Balozi Professa Costa Ricky Mahalu (Katikati) akizungumza na Mwenyekiti mteule wa SAUT Alumni Ndugu Pius Lufutu (Kushoto) pamoja na Mwanasheria wa Chuo Padri Claudius Nkwera.
**
Na Mwandishi wetu, SAUT
Chuo kikuu cha
Mtakatifu Agustino (SAUT) kampasi ya Mwanza kinatarajia kuzindua umoja wa
wanazuoni (Alumni) waliowahi kuhitimu chuoni hapo toka kuanzishwa kwake.
Hayo yamejiri hapo jana
pindi viongozi wakuu wa chuo hicho walipokutana kwa ajili ya kikao cha awali kujadili
uanzishwaji wa SAUT Alumni mnamo mwezi Aprili.
Akizungumza mara baada
ya kikao hicho, Mwenyekiti mteule wa umoja wa wanazuoni hao Pius Lufutu alisema
uzinduzi rasmi wa Alumni ni kwa ajili ya kuwatambua wanazuoni wote waliowahi
kuhitimu chuoni hapo pamoja na wao kushiriki katika kuendeleza chuo kupitia
miradi mbalimbali.
“Uzinduzi wa Alumni hii
itakuwa ni kwa ajili ya kuwatambua wanazuoni wote waliowahi kuhitimu chuoni hapa
iwe wapo ndani ya nchi ama nje ya mipaka. Lengo likiwa ni kuwahamasisha
kushiriki katika katika kuendeleza miradi itakayo chochea maendeleo ya chuo
kama namna yao kuonesha fadhila,” alisema.
Aidha pamoja na hayo,
Lufutu alisema chuo pia kitawasaidia Alumni hao kuwatafutia fursa mbalimbali
pamoja na kushirikiana nao kwa ukaribu ili kuweza kuchochea maendeleo yao.
Kwa upande wake Makamu
Mkuu wa Chuo SAUT, Balozi Professa Costa Ricky Mahalu alitoa wito kwa Alumni
kuweza kuwa tayari kushiriki kikamilifu huku ikitarajiwa Alumni kuwa ni kwa
ajili ya manufaa ya wote.
“Nina imani kabisa
kwamba uzinduzi wa Alumni utawanufaisha wengi, ikiwemo pia kuisaidia jamii ya chuo
chetu hiki. Hivyo ni wito wangu kwamba wanazuoni wahitimu watakuwa tayari kwa
ajili ya kuking’arisha chuo chetu na kukifanya kuwa sehemu endelevu ya kupata
elimu bora katika mazingira wezeshi,” alisema Profesa Mahalu.
Social Plugin