Mhasibu wa Manispaa ya Shinyanga Seif Hamad Mande amefariki dunia leo jioni Alhamisi 18,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila amethibitisha taarifa za kifo cha Seif Hamad Mande akieleza kuwa alikuwa ameugua kwa muda mrefu.
Seif Hamad Mande amewahi kuwa Mweka Hazina wa timu ya Stand United na amekuwa Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Rafiki SDO linalojihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto na masuala mbalimbali ya kijamii
Mungu ailaze Mahali pema peponi roho ya marehemu Seif Hamad Mande. Amina.
Social Plugin