Seneta wa Garissa nchini Kenya Mohamed Yusuf Haji amefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan, mjini Nairobi ambako alikuwa anapata matibabu, kwa mujibu wa familia yake.
Bwana Haji pia alikuwa mwenyekiti wa Jopokazi la Maridhiano nchini Kenya maarufu kama BBI (Building Bridges Initiative).
Bwana Haji alijiunga na utawala wa maeneo nchini Kenya mwaka 1960 kama mkuu wa wilaya na kupanda ngazi hadi kuwa miongoni mwa makamishna maarufu mikoani.
Bwana Haji alistaafu katika uongozi wa utawala wa mikoa mwaka 1998.
Mwaka 2002, aliteuliwa kuwa mbunge na mwaka 2007, akachaguliwa kama mbunge wa eneo la Ijara kwa tiketi ya chama cha Kenya African National Union (Kanu).
Wakati wa kifo chake, Bwana Haji alikuwa anahudumu muhula wake wa pili kama seneta wa Garissa.
Chanzo- BBC Swahili
Social Plugin