Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mpira Miguu mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Said Mankiligo
Katibu mpya wa Chama Cha Mpira mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Maiko Kaijage
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira manispaa ya Shinyanga Ibrahimu Kani ambaye amechaguliwa kuwa mwakilishi wa mkutano mkuu mkoa wa Shinyanga.
***
Na Suzy Luhende, Shinyanga
Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) kimefanya uchaguzi wake na kumchagua Said Mankiligo kuwa mwenyekiti wa chama hicho ambaye ataongoza kwa kipindi cha miaka minne.
Awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Benester Lugola ambaye hivi karibuni alifungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na makosa ya kinidhamu.
Uchaguzi huo umefanyika leo Februari 17, 2021 katika ukumbi wa mkoa wa Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga James Malima kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Akitangaza matokeo mwenyekiti kamati ya uchaguzi SHIREFA Thomas Mtani alisema idadi ya wajumbe wenye sifa ya kupiga kura ilikuwa 17 na hakuna kura iliyoharibika, nafasi ya mwenyekiti walikuwa wagombea wawili Salumu Kitumbo alipata kura saba (7) Said Mankiligo alipata kura (10) ambaye ndiye aliibuka mshindi.
Mtani alisema katika nafasi ya katibu waligombea watu watatu ambapo Maiko Kaijage alipata kura 10 as mbaye pia allibuka kidedea, wajumbe waliochaguliwa ni Ibrahimu Kani ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mpira Kahama amekuwa mwakilishi wa mkutano mkuu, Ibrahimu Magoma amechaguliwa kuwa mwakilishi wa virabu na Christina Rwekiza kachaguliwa kuwa mweka hazina wa chama hicho.
Baadhi ya wanachama wa chama mpira mkoa wa Shinyanga Jeremiah Igulu ambaye ni mwakilishi wa manispaa ya Kahama amesema mchakato wa uchaguzi ulikuwa mzuri japo kulikuwa na makandokando ambapo wa wanachama kutoka Manispaa ya Kahama walitaka kukataliwa kupiga kula kwa madai kuwa si wajumbe halali.
"Tunamshukuru Mungu kwa sababu uchaguzi umefanyika kwa amani ijapokuwa tulitaka kukataliwa kupiga kura sisi wa kutoka Kahama lakini baadae tulikubaliwa na tukapiga kura, hivyo tunaamini viongozi tuliowachagua watafanya vizuri kwa sababu wana uchungu na timu zao za mkoa ziweze kupanda madaraja",alisema Fadhili Kipindula.
Kwa upande wake mwenyekiti aliyechaguliwa Said Mankiligo wakati akiwashukuru wanachama amesema anashukuru kwa kumwamini, hivyo nia yake ni kunyanyua vilabu nakutafuta wadau ili kuupandisha mpira wa miguu katika mkoa wa Shinyanga.
Mankiligo ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa chama cha mpira kwa wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo vilabu alivinyanyua kwa kuwatumia wadau na juhudi zake binafisi sababu mchezo wa mpira uko moyoni mwake pia ameahidi kupandisha timu zote za mkoa ziweze kupanda madaraja na kufanya vizuri.
Mankiligo amesema kuwa atakacho kifanya ni kuhakikisha anatafuta wadau mbalimbali ili kusaidia kuzinyanyua timu za mkoa wa Shinyanga.
“Kwa sasa mmeniamini nitahakikisha nafuata katiba na utaratibu uliowekwa na TFF kwanza nitataka watu wajue suala la mapato na matumizi kwa kuwaitisha kila mwaka mkutano mkuu kwani mkutano kipindi hiki kinachopita haukuwahi kuitishwa na hilo sitaki kulizungumzia zaidi” amesema Mankiligo.
Aidha amesema kuwa anaahidi kufanya kazi kwa utaratibu na sheria na timu ya zamani ya stendi United Shinyanga itaundwa upya, na timu ya Mwadui atahakikisha inapanda madaraja na kutoka hapo ilipo, kuwanyanyua waamuzi wanawake na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 vitu ambavyo havipo kwa sasa.
"Nawashukuru sana wajumbe wangu mlionichagua na wale ambao hamkunichagua hivyo mmenipa kazi ya kufanya kwanza nitahakikisha timu ya standi united mpya naiunganisha na timu ya stend kampuni inakuwa kitu kimoja ili iweze kuwa chama kimoja chama lawana mambo yaende vizuri",alisema Mankiligo.
Naye katibu wa chama cha mpira wilaya ya Shinyanga vijijini Laurence Manota amesema anawashukuru wajumbe kwa kuchagua watu wanaojitoa kufanya kazi kwa ajili ya michezo hivyo anaamini watafanya vizuri watasaidia timu zote kupanda, na lengo ni kupandisha mpira Shinyanga.
Maiko Kaijage ambaye amechaguliwa kuwa katibu amesema wananchi wa mkoa wa Shinyanga wategemee utumishi uliotukuka hivyo wapewe muda tu watafanya vizuri.
Social Plugin