Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FAMILIA YAPATA PIGO KWA KUPOTEZA NDUGU WANNE MFULULIZO...MAMA, BABA WAPISHANA SIKU TATU TATU

Profesa Delphina Mamiro enzi za uhai wake

***
Nchini Tanzania , Familia moja ya mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), mkoani Morogoro Profesa Delphina Mamiro imepata pigo ndani ya mwezi mmoja kwa kupoteza watu wanne mfululizo ndani ya familia moja, Gazeti la Mwananchi limeripoti.

Profesa Delphina, mume wake na wazazi wake wote , mama na baba yake wamefariki pia kwa kupishana siku tatu tatu.

Profesa Delphina alianza kujisikia vibaya mwanzoni mwa mwezi huu na kufariki dunia akipatiwa matibabu hospitali na siku chache baadaye mumewe alifariki dunia.

Wazazi wake Delphina walifariki Januari 13 na 16,mkoani Kilimanjaro ,Moshi na hivyo Profesa huyo na mume wake walitoka Morogoro na kwenda kuzika.

Lakini baada ya kurudi , wote wanandoa hao waliugua na kufariki dunia.

Vifo vyao ni miongoni mwa vifo vilivyoibua hisia mbalimbali nchini Tanzania, wakati ambapo zimekuepo taarifa nyngi kuhusu watu kupoteza ndugu na jamaa zao siku za hivi karibuni.

Awali, wazazi wa profesa huyo walifariki dunia katika familia Januari mwaka huu wakipishana siku tatu, baada ya kuanza mama yake na kufuatiwa na baba yake.

Hata hivyo, wakati machungu hayo hayajapoa, Profesa Delphina alianza kujisikia vibaya mwanzoni mwa mwezi huu na kufariki dunia akipatiwa matibabu hospitali na siku chache baadaye mumewe alifariki dunia.
Dk Peter Mamiro

Akizungumza na Mwananchi jana nyumbani kwa marehemu eneo la Kihonda Manispaa ya Morogoro kabla ya kukataa kuzungumza zaidi, Anna Mamiro, ambaye ni mtoto wa Profesa Delphina, alisema vifo vya wazazi wao ni pigo kwa familia.

Anna alisema Januari 13 mwaka huu mkoani Kilimanjaro walimpoteza bibi yao mzaa mama aliyemtaja kwa jina la Franciska Kyessi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Alieleza kuwa wakati wakiombeleza kifo cha bibi yao, Januari 16, mwaka huu wakapata pigo jingine la kifo cha babu yao mchungaji Lucas Kyessi, ambaye alifariki ghafla.

“Mama na baba walitoka Morogoro na kwenda Moshi kwa ajili ya kuzika na baada ya hapo walirejea Morogoro na kuendelea na majukumu yao.

“Hata hivyo, baada ya siku chache mama akawa analalamika hajisikii vizuri. Baadaye akaugua na ikabidi kumpeleka hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi,” aliongeza Anna.

Anna alisema mama yao alifariki Jumamosi iliyopita, Februari 6, huu baada ya kuzidiwa.

“Wakati tukiendeleza maandalizi ya mazishi na kusafirisha mwili wa mama kwenda mkoani Kilimanjaro, usiku wa kuamkia Februari 9 (jana) mwaka huu, tukapata msiba mwingine mzito wa baba yetu,” alisimulia Anna.

Alisema Dk Peter Mamiro alifariki dunia nyumbani kwake maeneo ya Veta Kihonda baada ya kuugua kwa muda mfupi.

 Chanzo Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com