Picha ya nyanya
**
Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Mkazi wa kijiji cha Urauri ,kata ya Reha wilayani Rombo mkoa wa Kilimanjaro Magreth Mushi ameuawa kwa kukatwa Panga 'kitu chenye ncha kali' kichwani na kaka yake aitwaye Neoni Lazaro kwa madai ya kugombania fedha alizouza nyanya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amesema tukio hilo limetokea Februari 9, 2021 saa tatu usiku katika kijiji cha Urauri kata ya Reha wilayani Rombo.
Amesema Magreth alifariki dunia usiku huo wa kuamkia Februari 10 alipopelekwa katika Hospitali ya Huruma kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Social Plugin