Kamanda wa polisi katika jimbo la Kano Kaskazini mwa Nigeria amethibitisha kifo cha Mustapha Muhammad, mkazi wa kijiji cha Malam Na Andi, ambaye amedaiwa kujiua kwa chupa.
Polisi imesema kuwa mwanaume huyo aliamua kujiua kwa njia hiyo baada ya kujifungia ndani ya nyumba katika eneo la Masukwani katika jimbo la Kano kwa kupanda kwenye dirisha la nyumba yake, kabla ya kukata sehemu zake za siri.
Msemaji wa polisi katika jimbo la Kano DSP Haruna Kiyawa amesema kuwa tukio hilo lilitokea Jumapili, Februari 14,2021 ambapo walipokea ripoti kuwa kijana alikuwa amejifungia ndani ya nyumba katika eneo la Musukwani huku akiwa na chupa mkononi mwake.
DSP Kiyawa aliongeza kuwa kijana huyo aliingia ndani ya chumba na kukata uume wake na kujidunga kwa chupa alilokuwa amelivunja upande mmoja na katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.
"Muda mfupi baada ya kupokea taarifa, polisi waliwasilikatika nyumba hiyo na akapelekwa hospitalini ya Murtala iliyopo mjini humo, ambako alitangazwa na madaktari kuwa amekufa wakati madaktari walipokuwa wakijaribu kuyanusuru maisha yake," alisema msemaji wa polisi Kiyawa.
BBC ilimnukuu mmoja wa wanawake wanaoishi katika eneo hilo akisema: "Tuliamka asubuhi kuendelea na kazi zetu za siku ndipo tulipomuona kijana huyu akikimbilia ndani ya nyumba yake. Hakwenda mahali mahali popoteisipokuwa ndani ya chumba cha mama yangu. Mara akafunga chumba.
"Huko ndio alikokutwa ameumia na alikuwa amejikata pia kwenye paji lake la uso, alikuwa akitokwa na damu nyingi.
Usman Umar, mmoja wa marafiki wa marehemu, pia ameiambia BBC kuwa alimsikia akiongea na mtu ambaye hakuonekana, saa kadhaa kabla ya kujiua, huku akiwa amevaa kaptula huku akizozana na mwanaume mwingine lakini hakumuona.
"Amekuwa rafiki yangu tangu tulipokuwa watoto, na alikuwa mtu mwema sana. Nilimuona akizozana na mlemavu aliyesema kuwa wengine wanawasaidia maskini lakini yeye hafanyi hivyo.
"Alikuwa akisema miguu yake ilikuwa imepooza na akamwambia kwamba alitoka nje ya nyumba akitaka kumuangamiza.
"Hatukujua alikuwa anamaanisha nini. Nilimshawishi nikamsihi aende nyumbani akavae nguo. Halafu akaondoka, vinginevyo hatukujua ni nini kingetokea ," alisema rafiki yake.
Ibrahim Abdusallam, kaka yake mdogo wa marehemu Mustapha, pia alisema kuwa alikuwa na ugonjwa wa akili wakati mmoja alipotoka Saudi Arabia, na siku tatu kabla ya kifo chake maradhi yalikuwa yamerejea na alikua katika hali mbaya zaidi.
Hii ina kuja baada ya mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha FUD Dutsen, kilichopo katika jimbo la Jigawa nchini humo kupatikana akiwa amekufa baada ya malumbano na mpenzi wake wa kike.
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin