Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt. Emmanuel Makala
***
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt. Emmanuel Makala
amewaongoza waumini wa kanisa hilo Usharika wa Ebenezer mjini Shinyanga katika
uzinduzi wa siku tatu mfululizo za kufunga na kuomba zinazoenda sambamba na
siku 40 za mfungo wa Kwaresma kwa lengo la kuitikia wito wa Rais Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli kuwataka Watanzania kufanya maombi ya kuliombea taifa kwa
mwenyezi Mungu awaepushie Watanzania ugonjwa wa Corona.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
maombi hayo Askofu Dkt. Emmanuel Makala amesema kiongozi wa nchi anapoagiza
kitu au anapotoa rai wa wananchi asiyepokea na kutii atakuwa anapingana na
ofisi na siyo mtu kwa hiyo yeye ameitikia wito wa kiongozi wa nchi na kuwataka
waumini wa dini ya kikristo pamoja na dini zingine kuungana na Watanzania
wengine kuomba na kuliombea taifa kwa mwenyezi Mungu kuiepusha nchi na ugonjwa
huu wa Corona.
Aidha Chaplain wa Kanisa Kuu la Ebenezer na Mchungaji Kiongozi Mch. Odolous Gyunda amesema
lengo la maombi ya siku tatu mfululizo ni kutubu na kuabudu kwa ajili ya nchi
ya Tanzania na kumuunga mkono kiongozi wa nchi na maombi hayo yanayoambatana na
nyimbo za kusifu na kuabudu yataendelea kwa muda wa siku 40 za Kwaresma.
Baadhi ya waumini walioshiriki
katika ibada hiyo ya maombi wamesema wanamuona Mheshimiwa Rais Dkt. John Joseph
Pombe Magufuli kama mfalme wa Ninawi enzi zile alipopiga mbiu kumlilia Mungu na
kuomba toba kwa hiyo sauti aliyoutoa Rais ni sauti ya Mungu kwa ajili ya
kuliokoa taifa la Tanzania.
Naye Katibu wa Dayosisi Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria bi. Happyness Gefi kama kungelikuwa na namna rahisi
ya kuponyesha ugonjwa wa Corona basi mataifa makubwa yenye nguvu na uwezo
yangekuwa yameshatokomeza ugonjwa huo kwa uwezo wa kiuchumi walio nao lakini
lakini kwa kuwa ugonjwa huo haubagui tajiri wala masikini ni jambo la
kumshukuru mungu sana kwa maono aliyo nayo lakini pia shukrani kwa Askofu
Emmanuel Makala kwa kuona umuhimu wa kupokea wito wa mkuu wa nchi na kushusha
chini kwa waumini kutekeleza kwa vitendo kwa nia moja na kwa dhati ya mioyo
yao.
Social Plugin