Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya, limefanikisha kuipata bastola ya mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye, iliyoibiwa nyumbani kwake maeneo ya Kawe.
Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 18, 2021, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa, na kusema kuwa bastola hiyo iliibiwa Februari 15, 2021, majira ya saa 11:00 alfajiri nyumbani kwake maeneo ya Kawe.
Aidha SACP Mambosasa ameongeza kuwa bastola hiyo aina ya GLOCK 17 yenye No. YX647 ikiwa na risasi 14 ndani ya kasha lake, imekamatwa jana mkoani Mbeya na mtuhumiwa wa wizi wa silaha hiyo anashikiliwa na jeshi la polisi.
Social Plugin