Mkuu idara ya mawasiliano ya Uhandisi na elektroniki UDOM, Dkt Florence Rashidi
**
Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainabu Chaula amesema juhudi za pamoja zinahitajika kutengeneza , mazingira ya kukuza matumizi bora ya mawasiliano nchini.
Dkt.Chaula amesema hayo leo Februari 23,2021 jijini Dodoma katika Kikao cha kujadili Mkakati wa TEHAMA kwenye ngazi ya jamii ikiwemo vituo vya Afya na shule hapa nchini ,Tanzania Community Digitization[TCD]kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Mawasiliano.
“Juhudi hizi za pamoja zitatusaidia katika kukuza sekta ya mawasiliano zikiwemo ni pamoja na mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hii ni katika kuhakikisha mawasiliano yanafika katika ngazi zote hadi vijijini”amesema.
Aidha,Dkt. Chaula amesema moja ya malengo ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni kuhakikisha taasisi zote za umma zinapata huduma ya Mawasiliano kwa gharama nafuu ifikapo mwaka 2025 wizara itajipima angalau kufikia asilimia 40% .
Hata hivyo, Dkt.Chaula amebainisha kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga ni kwa namna gani inahakikisha inafikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali ambapo wizara imetoa mwelekeo katika kusambaza huduma ya mawasiliano.
“Ndio maana serikali ina sera ya TEHAMA ya mwaka 2000 na mwaka 2016 serikali ilipitia sera ili kwendana na mazingira na maendeleo ya Teknolojia ,lazima tutengeneze mazingira ya Evaluation mwezi uliopita umefanya nini na sasa unafanya nini,na tunatambua mchango wa sekta binafsi katika mawasiliano hivyo tumejipanga katika kuhakikisha sekta ya mawasiliano inasonga mbeleamesema.
Pia , Dk.Chaula amesema vyombo vya Habari vina mchango mkubwa katika kuhabarisha umma juu ya umuhimu wa mawasiliano katika kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa mifumo ya Habari USA, Desden Wengaa amesema wataendelea kushirikiana na Wizara katika Nyanja mbalimbali za mawasiliano.
“Kwa nanma moja ama nyingine wote tunahusika na jambo hili ,tumejenga mifumo mikubwa TAMISEMI ,kupitia level za halmashauri mpaka level za vijiji ,ili mifumo ifanye kazi vizuri lazima internet connection”amesema.
Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Munaku amesema pamekuwepo na changamoto ya wadau wengi kupeleka huduma ya mawasiliano katika sehemu moja na wengine kukosa huduma hiyo .
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya kutoa majukwaa ya mtandao wa kujifunzia kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari[Shule Direct] Faraja Nyarandu amesema mradi huo umekuja kwa muda muafaka katika kukuza sekta ya mawasiliano nyanja za elimu huku mkuu wa idara ya mawasiliano ya uhandisi na elektroniki kutoka chuo kikuu cha Dodoma Dkt.Florence Rashidi akibainisha wamejipanga kushirikiana serikali .