Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Zainab Chaula akizungumza wakati akifunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi ,akizungumza wakati wa kufunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.
Posta masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe,akielezea jinsi walivyojifunza mafunzo hayo kwa siku tatu wakati wa kufunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainabu Chaula (hayupo pichani) wakati akifunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainabu Chaula amelitaka baraza la wafanyakazi wa shirika la posta Tanzania kufanyakazi kwa weledi na kuweka mikakati ya kuhakikisha shirika hilo linajiendesha kwa faida na kuchangia uchumi wa taifa.
Dkt Chaula ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini waliokutana kujadili na kutathmini utendaji kazi wa shirika hilo katika utendaji kazi wake.
Amesema ni wajibu wa kila mtumishi ndani ya shirika hilo kuhakikisha anafanyakazi kwa bidii na kuongeza tija katika shirika na kuongeza uzalishaji kama ilivyokusudiwa wakati wa uanzishwaji wa shirika hilo.
"Kila mtu ndani ya shirika ajitathmini amelifanyia nini shirika, kila taasisi imewekewa target ataongeza vipi ajira mpya za ndani kama nchi tumejiwekea ajira milioni nane 8,000,000 kati ya hizo je taasisi yako itatoa ngapi" amesema Dkt Zainabu Chaula.
Aidha Dkt.Chaula amelitaka shirika kujitathmini katika utendaji kazi wao katika Mkoa yote kuhakikisha Mikoa yote inafanya vizuri na kusaidia Mikoa ambayo haifanyi kazi vizuri ili nayo ifanye kazi vizuri.
Dkt.Chaula amesema kuwa kwa sasa utendaji kazi wa shirika unazidi kuimarika hivyo kila mtumishi kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuboresha zaidi huduma zinazotolewa na shirika la posta.
Aidha amewataka wajumbe wa baraza kwenda kuyatumia mafunzo waliyoyapata juu ya huduma mpya zilizoanzishwa na shirika na kuongeza mchango katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya mawasiliano.
Awali Posta masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang'ombe amesema baraza limekaa kwa siku tatu (3) likishirikisha watumishi kutoka ngazi mbalimbali kwa lengo la kutathmini na kuweka malengo katika kuimarisha utendaji kazi wa shirika la posta.
Aidha katika siku tatu hizo walipata wasaa wa kuchagua viongozi mbali mbali wa baraza na kupata mafunzo ya viashiria vya hatari katika uzalishaji wa shirika na kukuza uchumi wa nchi na utunzaji wa nyaraka za shirika.
Social Plugin