Askofu Emmaus Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Moravian
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuachia kwa dhamana Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Uamsho la Moravian baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwake.
Akizungumza leo Jumanne Februari 16,2021 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baada ya jeshi hilo kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake limemuachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
“Tumempuuza na baada ya kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, mchana huu tumemuachia kwa dhamana baada ya kutimiza masharti,” amesema.
Social Plugin