Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KAMATI YA USALAMA BARABARANI YAKABIDHI GARI LA MIL. 16 KWA JESHI LA POLISI SHINYANGA

Muonekano wa gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga itumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga imekabidhi gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga litumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.

Gari hilo limekabidhiwa leo Jumatatu Februari 8,2021 na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.

Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo, Majiji amesema gari hilo limetolewa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azimio namba 2 la Kongamano la Kitaifa la Usalama Barabarani lililofanyika Machi 30,2019 jijini Dar es salaam ambapo kila kamati ya mkoa ilielekezwa kununua gari ili kuongeza vitendea kazi kwa ajili ya kazi za usalama barabarani.

“Kamati ya Usalama barabarani mkoa wa Shinyanga imenunua gari lenye thamani ya shilingi Milioni 16 baada ya Mkaguzi wa magari kulikagua na kujiridhisha kwamba gari ni zima na linafaa kwa shughuli za usalama barabarani”,amesema Majiji.

Ameongeza kuwa gari hilo limepatikana kupitia michango mbalimbali ya wadau wakishirikiana na Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga.

Akipokea gari hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba ambaye ni mlezi wa Kamati ya Usalama Barabarani amesema wataitumia gari hiyo kwa shughuli za usalama barabarani,kupeleka askari polisi kwenye maeneo yanapotokea matukio barabarani na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya usalama barabarani.

“Tunaishukuru Kamati ya Usalama Barabarani kwa kutupatia gari hili. Gari hili ni chachu ya kupunguza matukio ya usalama barabarani na ninaahidi kusimamia kutunza gari hili”,amesema Kamanda Magiligimba.

Katika hatua nyingine amesema matukio ya ajali barabarani mkoa wa Shinyanga yamepungua kwani kati ya Januari hadi Desemba mwaka 2019 yaliripotiwa matukio 72  yaliripotiwa kati yake 34 ni ya vifo, 38 ya majeruhi ikilinganishwa na kipindi cha Januari hadi Desemba 2020 ambapo matukio 47 yaliripotiwa kati yake ya vifo ni 28 na majeruhi 19.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, ASP Africanus Sulle amesema watatumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kufika kwenye maeneo ya matukio na kutoa elimu ya masuala ya usalama barabarani ili kuhakikisha mkoa wa Shinyanga unapunguza ajali za barabarani.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji (kulia) akizungumza wakati wa kukabidhi gari aina ya Toyota Harrier lenye thamani ya shilingi Milioni 16 kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba leo Jumatatu Februari 8,2021. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akitoa taarifa ya manunuzi ya gari kwa ajili ya shughuli za usalama barabarani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akimkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba kadi ya usajili wa gari na vielelezo vyote vya gari aina ya Toyota Harrier.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha kadi ya gari na vielezo vyake.
Muonekano wa gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga itumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.
Muonekano wa gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga itumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.
Muonekano wa gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga itumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.
Muonekano wa gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga itumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akikata utepe kuzindua rasmi gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga itumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.
Wajumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani na Maafisa wa Jeshi la polisi wakipiga makofi baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba kukata utepe kuzindua rasmi gari aina ya Toyota Harrier yenye thamani ya shilingi Milioni 16 iliyotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga itumike wa ajili ya shughuli zote za Kikosi cha Usalama Barabarani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akionesha funguo ya gari aina ya Toyota Harrier wakati akimkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba.
Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Wilson Majiji akimkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba funguo ya gari aina ya Toyota Harrier.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Harrier.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Harrier.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza baada ya kupokea gari aina ya Toyota Harrier kutoka Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, ASP Africanus Sulle akizungumza baada ya makabidhiano ya gari aina ya Toyota Harrier lililotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga Jackton Koyi akizungumza baada ya makabidhiano ya gari aina ya Toyota Harrier lililotolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com