Polisi kutoka Athi River jimbo la Machakos nchini wanachunguza kisa ambapo mwanaume aitwaye Ernest Kamanda mwenye umri wa miaka 52 alizimia na kuaga dunia Jumatano, Februari 3,2021 usiku nyumbani kwa mwanamke aitwaye Catherine Kinyanjui.
Ernest Kamanda anasemekana alianza kukumbwa na matatizo ya kiafya majira ya saa 11:30 jioni Jumatano wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo.
Kulingana na ripoti ya polisi mwanamke huyo aliyetambulika kama Catherine Kinyanjui mwenye umri wa miaka 47, alimkimbiza mwanaume huyo katika hospitali ya Shalom akisaidiwa na majirani ambapo alisemekana alikata roho.
Inaelezwa kuwa alikimbizwa hospitali ya Shalom Community na majirani ambapo alisemekana tayari alikuwa amefariki dunia.
Polisi waliwasili eneo la tukio kutathimni kilichotokea huku mwili wake ukihifadhiwa katika makafani ya hospitali hiyo kusubiri upasuaji.
Visa vya wanaume kupoteza maisha yao wakila mahaba vimeripotiwa kuongezeka katika siku za hivi karibuni
Wiki mbili zilizopita mzee mwenye umri wa miaka 80 aliaga dunia katika njia isiyoeleweka akijivinjari na mrembo wa miaka 33 katika hoteli moja Dar es Salaam na mwaume mwingine akiwa na Gesti na mpenzi wake jijini Mwanza Tanzania.
Chanzo - TUKO
Social Plugin