JESHI LATANDA MITAANI, INTANETI YAZIMWA MAPINDUZI YA MYANMAR


Magari ya kivita yametanda katika mitaa ya miji kadhaa nchini Myanmar huku kukiwa na ishara kwamba wanajeshi wanaandaa msako dhidi ya wale wanaopinga mapinduzi yaliyofanywa Februari 1.

Mtandao wa interneti umezimwa nchi nzima licha ya juhudi za kimataifa kupinga hatua hiyo.

Katika jimbo la kaskazini la Kachin, vikosi vya usalama vimefyatua risasi katika siku ya tisa ya maandamano ya kupinga mapinduzi nchini kote.

Afisa  maalum wa umoja wa mataifa nchini humo amewashutumu wanajeshi kwa kile walichokiita kutangaza vita dhidi ya raia wasio na hatia.

Balozi mbalimbali za nchi za Magharibi zimehimiza jeshi kuonesha weledi wake wakati huu ambapo nchi hiyo ipo katika wakati mgumu.

Kote nchini humo, mamia ya maelfu ya waandamanaji wameendelea kujikusanya katika miji kadhaa ikiwa ni siku ya tisa mfululizo kupinga mapinduzi hayo.

 

-BBC



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post