MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema
Lugangira |
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema
Lugangira amesema hatua ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe
Rais Dkt John Magufuli kwa kufuta tozo 168 zilizohusu Kilimo,Mifugo na
Uvuvi na Biashara itasaidia kuimarisha uwekezaji na kunufaisha wakulima
wadogo nchini.
Neema
aliyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati alipopata nafasi ya
kuchangia katika Hoja ya Hotuba ya Mhe Rais Dkt John Magufuli ambapo
katika hotuba yake kwenye ukarasa wa 25 alisema katika miaka mitano
iliyopita alifuta tozo 168 .
Alisema
kati ya hizo 114 zilihusu kilimo,mifugo na uvuvi na 54 za biashara na
wataendelea na hatua hizo mwisho wa kumnukuu ambapo alisema jambo hilo
litasaidia kuimarisha uwekezaji na kunufaisha wakulima wadogo kupitia
mapato,
Mbunge Neema
alisifu jitihada ambazo zinafanywa na Serikali ya awamu ya tano kwa
kufanikisha hilo huku akiishauri serikali kufanya tathimini ili kuweza
kujiridhisha punguzo za tozo hizo kama pia zinawanufaisha wakulima
wadogo kama wanavyotarajia.
Aidha
aliiomba Serikali iagize wadau wote kufanya tathimini ya tozo zote
zilizotolewa maana kwa uzoefu wake unaonyesha kwamba wakati mwengine
tozo hizo hazina matokeo ya haraka kufika kwa wakulima wadogo ipasavyo.
“Nikushukuru
sana Mh Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami pia niweze kuchangia
hotuba ya Mhe Rais napenda kujielekeza kwenye sekta ya kilimo na hivyo
naamini uimarishaji wa mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara unatakiwa uende
sambamba na unufaikaji wa wananchi”Alisema
Alisema
jambo la pili katika Hotuba ya Mhe Rais ambalo angependa kuchangia ni
katika hotuba yake kwenye ukurasa wa 26 ambapo amesema kwamba kwa msingi
huu kwenye kilimo wanakusudi kuongeza tija na kufanya kiweze kuwa cha
biashara lengo ni kujihakikishia usalama wa chakula.
“Lakini
pia Mhe Rais alielekeza upatikanaji wa malighafi za viwandani na pia
kupata ziada ya kuuza nje ili kufanikisha hayo ntutahakikisha zana bora
za kilomo ikiwemo mbegu,viwatilifu ,mbolea,uukuaji dawa na matrekta
vinapatikana kwa beii nafuu”
Mbunge
huyo aliendelea kuipongeza serikali kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa
kipindi cha miaka mitano iliyopita na hotuba ya Rais imesisitiza yale
yaliyoandikwa kwenye Ilani ya CCM katika kifungu 35 hadi 46 hivyo ili
tuweze kufanikisha hayo kwa kasi angependa kushauri yafuatayo.
Alisema
cha kwanza ni lazima wajikite kwenye uzalishaji wa aina mbalimbali za
mbegu maana hivi sasa ukienda kwenye duka la mbegu utakuta asilimia 80
zimetoka nje ya nchi.
Ambapo
katika hilo aliishauri serikali kuzijengea uwezo taasisi za ndani na
binafsi za ithibati (local certification bodies) kwani kufanya hivyo
tutaweza kufanikisha mbegu tunazozalisha hapa nchini nazo ziweze kuuzwa
nje ya nchi.
Hata hivyo
alisema kwamba amekubaliana na mapendezo yaliyopo kwenye ilani ya CCM
kuhusu Wizara ya kilimo kuwa na bodi ya mazao na taasisi ambazo
zinahitaji kupitiwa upya kimuundo ili ikiwezekana kuwa na taasisi chache
zitakazoongeza ufanisi na usimamizi wa sekta hiyo.
Alisema
hivyo kwa sababu wingi wa hizo bodi za mazao na taasisi unaleta
mkanganyiko mkubwa kwenye sekta hivyo unakinzana na dhana nzima ya
kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekzaji na biashara kwa ujumla,
Mbunge
Neema alitoa wito kwa wadau wa sekta ya kilimo kuwa mstari wa mbele
kuhamaisha uzalishaji na ulaji wa vyakula nyenye viini lishe vingi ili
kuungana na juhudi za serikali kutokomeza udumavu na utapiamlo kwa
ujumla.
“Kama
tunavyofahamu Tanzania asilimi 32 ya watoto chini ya miaka 5 wamedumaa
kwa hiyo kila watoto 100 watoto 32 wamedumaa na inashangaza kwamba mikoa
inayoonza kwa hali hiyo inaongozwa kwa uzalishaji wa chakula” Alisema
Mbunge huyo.
Hata hivyo
alitoa wito kwa wadau hao pamoja na kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya
kibiashara badala yake wahamasishe ulaji wa mazao yenye viini lishe
vingi ambayo ipo kwenye Ilani ya CCM
Mwisho
Social Plugin