Na Dixon Busagaga -Kilimanjaro
SERIKALI mkoani Kilimanjaro imepiga chapuo kwa wawekezaji
nchini kununua hisa za Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) ili kuongeza
mtaji hadi kufikia sh Bil 100 utakao saidia benki hiyo kuwa benki ya kitaifa
kwa kusogeza huduma zake katika nchi nzima.
Hatua hiyo inatokana na Benki ya KCBL kuanza upya utoaji wa
huduma baada ya changamoto mbalimbali ilizopitia na kupelekea kunusurika kuwa
miongoni mwa Benki zilizofutwa na Benki kuu baada ya wadau na viongozi wa
serikali kuweka juhudi za kuinusuru.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuiga Bodi ya
Wakurugenzi wa benki hiyo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira alisema
“Sisi ni mashahidi watu wameanza kuingia na kutoka ndani ya
Benki na Benki inafanya vizuri ,tumeletewa wataalamu wazuri sana katika masuala
ya benki ,na wanasimamaia utaratibu vizuri fedha zinazoingia na fedha zinazotoka
lakini yutahitaji kukuza mitaji “alisema Dkt Mghwira
“Lengo letu sisi lilikuwa ni kufikia Bil 100 angalau ,uwe
mtaji wa kuanzia kwa hiyo tulikuwa tunatafuta wawekezaji wakubwa ambao
wangeweza kununua asilimia ishirini ,ishirini za Bil 20 za hisa kama watatu
wanne ,ambao tulikuwa tunategemea kwa njia hiyo tungeweza kupata wawekezaji
wakubwa “aliongeza Dkt Mghwira .
Alisema serikali bado inaendelea kuwatafuta na kwamba upo
uwezekana wakapataikana baada ya baadhi ya benki kubwa kuonesha nia ya kununua
hisa katika benki hiyo hatua itakayosaidia kuongeza mtaji wa benki .
Meneja Mkuu wa Benki hiyo Godfrey Ng’ura alisema changamoto
zilizokuwepo awali katika benki hiyo kwa
sasa zimemalizkka na kwamba tayari huduma imeanza kutolewa ambapo katika
kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo
tayari akaunti mpya zaidi ya 200 zimefunguliwa .
“Benki inamtaji na ukwasi wa kutosha ,tumeemndelea kuwalipa
wateja wetu amana zao , na watejawameendelea kufungua akaunti ,katika miezi
mitatu tumefungua akaunti mpya zaidi ya 200 zenye thamani ya zaidi ya Mil 600
na tumefanya malipo katika amana za wateja ndani ya miezi mitatu zaidi ya
Bilioni 2”alisema Ng’ura .
Benki ya Ushirika Kilimanjaro ilizinduliwa kwa mara nyingine
hivi karibuni baada ya kuingia mkataba wa makubaliano na Benki ya CRDB ambapo imefanya uwekezaji wa shilingi Bilioni
7kwa lengo la kuimarisha utendaji wa benki ya ushirika.
Social Plugin