NAIBU
Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo bungeni |
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia NGOs Mh .Neema Lugangira akiuliza swali bungeni
MWANDISHI WETU, DODOMA.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora;
Mhe Deogratius Ndejembi amesema Serikali tayari imeanzisha kanzidata kwa
walengwa wote wanaopokea fedha za TASAF ambao ulianza kwa Halmashauri
19 nchini lakini kwa sasa umekwisha kuzifikia Halmashauri 39.
Aliyasema
hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali mawili ya ya nyongeza
ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kupitia NGOs Mh Neema Lugangira ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango
gani wa kuanzisha kanzidata kwa kutumia Tehama ili kuhakikisha
wanufaika wa mpango wa TASAF ni wale waliokidhi vigezo ambavyo
vimewekwa.
Sambamba na
kuondoa mianya ya watu wanaonufaika na mpango huo kusajiliwa mara mbili
kwenye maeneo tofauti tofauti jambo ambalo linapelekea wengine kukosa
fursa hiyo muhimu.
Naibu
Waziri huyo alisema pia wataanza kuweka mfumo wa kuunganisha kanzidata
na NIDA na mitandao ya simu ili walengwa badala ya kupokea fedha
dirishani kwa wale wanaoenda kugawa fedha hizo ziende moja kwa moja
kwenye simu zao ili kuhakikisha hakuna malipo mara mbili.
Alisema
kwa sababu kumekuwa na malalamiko kwamba watu wanapokea mara mbili
fedha na hata mtu akiwa hayupo zinachukuliwa na watu wengine hivyo ili
kudhibiti hilo lisiendelee kutokea ndio maana watakwenda kuweka mfumo
huo kwenye Halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na maeneo ya Uguja na
Pemba.
Katika swali lake
la pili Mbunge Neema aliuliza Je serikali ina mpango gani kuhakikisha
kaya ambazo hazikunufaika awali sasa zinanufaika kwenye awamu ya tatu ya
TASAF hususani wazee sio tu kwa Manispaa ya Bukoba bali pia mkoa wa
Kagera na Taifa kwa Ujumla.
Akijibu
swali la pili la Mbunge huyo, Naibu Waziri huyo alisema Serikali
itatanua mpango huu kwa wazee ambao hawakuingia na kaya ambazo
hazikuingia wataingia hivyo aliwatoa mashaka wabunge wa majimbo na viti
maalum nchini kuwa mpango huo unakwenda kwenye kaya milioni 1.4 ambazo
ni sawasawa watu milioni 7 ambao watakwenda kunufaika na mpango huu wa
TASAF.
Social Plugin