Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John William Kijazi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021. PICHA NA IKULU
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi wakati wa kuaga
mwili wake katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa
Februari 19, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John William KijaZi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021
Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Bi. Dorothy Mwaluko wakibeba shada la maua lenyen herusi KMK yaani Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi
Balozi John William Kijazi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021.
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi wakati wa kuaga mwili wake katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapimnduzi ya Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi wakati wa kuaga mwili wake katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA Mhe. Allan Kijazi akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi wakati wa kuaga mwili wake katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa
Februari 19, 2021 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akitoa heshima zake za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John William Kijazi wakati wa kuaga mwili wake katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19, 2021.
Rais Magufuli akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Balozi John Kijazi wakati wa ibada ya kuaga mwili huo kwenye viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa amekaa kwa majonzi wakati mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ulipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19,2021 ambako ameongoza shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mara baada ya kumalizika kwa ibada ya kuaga.
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete wa pili kutoka kushoto , Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Naibu Spika wa Bunge Mh.Dk. Tulia Ackson Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mh. Hemedi Suleiman Abdallah kulia ni miongoni mwa waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Ijumaa Februari 19,2021.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk.Bashiru Ali na Waziri wa Sheria na Katiba Dk.Mwigulu Nchemba wakiwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi John Kijazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Kamishna mkuu wa Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi kulia akiwa pamoja na Ndugu na jamaa wakati wa kuaga mwili wa ndugu yao mpendwa Marehemu Balozi John Kijazi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo.
Mwili wa Marehemu Balozi John Kijazi ukiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo shughuli za kuaga zimefanyika kabla ya kwenda Korogwe Mkoani Tanga kwa mazishi.
Mwili wa Marehemu Balozi John Kijazi ukiwasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam ambapo shughuli za kuaga zinafanyika kabla ya kwenda Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi.
Baadhi ya Makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali wakipita na kutoa heshima zao za mwisho kwa Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi John Kijazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaongoza waombolezaji na Watanzania wote kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John William Herbert Kijazi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli amesema Kijazi ameondoka hapa Duniani kama shujaa na Maalim Seif ameondoka hapa duniani kama shujaa hivyo tuwaenzi na kuyaamini mambo yao waliyoyatekeleza hapa Duniani kwa mapenzi makubwa.
“Familia ya marehemu Kijazi, Mama Kijazi ninakuomba ukaendelee kulisimamia hili ninajua wewe nimuombaji mzuri endelea kumuombea mume wako, watoto mkaendelee kujenga umoja ulioachwa na Baba yenu, ndugu na jamaa akiwepo mdogo wake kasimamieni hilo.
“Nakushukuru Mzee Kikwete kwa kuja, nawashukuru viongozi wote mliohudhuria hapa nakushukuru sana Baba Poroko, Mungu ambariki sana marehemu Kijazi huko aendapko najua na sisi tuko njiani tunakuja, Mungu aibariki familia,” amesema Rais Magufuli.
Baada ya kuagwa kwa taratibu za kiserikali, mwili utasafirishwa hadi Korogwe mkoani Tanga ambapo atazikwa siku ya Jumamosi.
Balozi Mhandisi John William Herbert Kijazi amekuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 - 2016 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.
Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.
Social Plugin