Kombe la Simba Super Cup
Klabu ya soka ya Simba SC imeibuka Mabingwa wa michuano ya Simba Super Cup baada ya kufikisha pointi 4 ambazo hazijafikiwa na washiriki wengine Al Hilal na TP Mazembe.
Mashindano hayo yamehitimishwa jana Januari 31, 2021 kwa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe ambao umemalizika kwa suluhu na Simba SC kuibuka mabingwa.
Mchezo wa kwanza ulipigwa Januari 27, 2021 ambapo Simba SC waliifunga Al Hilal magoli 4-1.
Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Al Hilal ambao waliifunga magoli 2-1 klabu ya TP Mazembe.
Mfungaji bora wa michuano amekuwa Bernard Morrison akifunga magoli mawili, huku mchezaji bora wa mashindano akiwa ni Rally Bwallya.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez, amesema kuwa kwa kiasi kikubwa malengo ya michuano hiyo yametimia ambayo ilikuwa ni kujenga utimamu kwa wachezaji kuelekea hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba ipo kundi A na timu za As Vita ya DR Congo, Al Ahly ya Misri na Al Merrick ya Sudan.
Social Plugin