WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa akisisitiza jambo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali papo kwa hapo ya wabunge |
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa ikitumia Balozi zake za
nje kutangaza mazao yaliypo ndani ya nchini ili kuweza kuyauza kwenye
nchi ambazo wanatumia mazao hayo hatua ambayo imepelekea kupata wateja
wengi kuja kununua hali iliyosaidia kuimarika kwa masoko.
Aliyasema
hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa hapo la
Mbunge wa Viti Maalumu ( CCM) kupitia NGOs Mh Neema Lugangira ambapo
aliuliza kutokana na uwepo tatizo kubwa la masoko ya mazao yaliyopo
nchini hata kama wakulima wanazalisha kwa ubora wa hali ya juu.
Je
Serikali ipo tayari kupelekea wataalamu wake kwenye nchi ambazo
zimefanikiwa ili kujifunza namna bora ya usimamizi wa masoko yaliyopo
Waziri
Mkuu Majaliwa alisema kwamba muhimu ni kutafuta mfumo mzuri unaowezesha
mazao yaliyopo kujulikana na kuyauza kwenye nchi ambazo kuna wateja na
wapate bei nzuri kama ilivyo ndani ya nchi uwepo mfumo wa stakabahdi
ghalani ambao unakusanya mazao pamoja na kuwaalika wanunuzi wanakuja
kila mmoja anatamka atanunua zao hilo kwa bei gani hivyo yule mwenye bei
ya juu anapata fursa kununua.
Alisema
kwamba huo ni ni mfumo uliondaliwa kwa ajili ya uuzaji wa mazao na
utakuwa na bei nzuri huku akieleza pia Serikali ina mpango wa kutafuta
masoko kwenye nchi ambazo zinazohitaji mazao hayo ili kuhakikisha
wakulima wananufaika na kuweza kujikwamua kiuchumi
“Juzi
nilikuwa na Wabunge wa Mkoa wa Rukwa wakiomba Serikali iwasaidie kufika
nchi ya Kongo, Zambia, Rwanda na Burundi kutafuta masoko ya mazao
yanayolimwa mkoani humo” Alisema Waziri Mkuu
Aidha
alisema kazi inayofanywa kwa sasa na Serikali ni kuhakisha inawasiliana
na nchi ambazo ni walaji wa mazao hayo ili kujihakikisha mazao hayo
yanapolimwa na kuvunwa yanapelekwa kwenye nchi zao na hiyo ni njia ya
kupata soko nzuri la mazao pamoja na ubora unaofanywa.
Alisema
kwa sasa Serikali itaendelea kujenga masoko ya kimkakati na ya kikanda
ambayo yanalengwa pembezoni mwa nchi ili kukaribisha waliopo jirani
kwenda kununua mazao yanayozalishwa hapa nchini
“Lakini
miezi mitatu iliyopita nilikuwa Kilimanjaro pale Holili wanajenga soko
kubwa sana ambalo wananchi wanaozalisha mazao yanapelekwa hapo na watu
wa nchi jirani watakwenda hapo kununua na wanawapunguzia ugumu wa
kuingia mpaka ndani”Alisema
Hata
hivyo alisema mwezi mmoja uliopita alikuwa mkoani Kigoma ambapo eneo
Kagunda wamejenga soko nzuri wanawakaribisha majirani watu wa Burundi na
Rwanda kwenye kununua jambo ambalo linapunguza umbali wa kufuata
bidhaa.
Sambamba
na hilo alieleza kwamba hivi sasa Serikali inajenga soko kubwa mkoani
Kagera eneo la Nyakanazi lengo wale wanaotoa Kongo, Rwanda watafika
kwenye soko hilo la zaidi ya Bilioni 3.5 ili waweze kupata bidhaa na
muhimu ni kuweka mkakati wa namna mazao yaliyoboreshwa na kupata thamani
kubwa ili yaweza kupata thamani kubwa ili kumuwezesha mkulima aweze
kupata tija kwa kazi ya kilimo anayoifanya.
Mwisho