WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Tanga kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica OmariWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Tanga kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella na kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica OmariKatibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari kushoto wakati wa ziara hiyo
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo
WAZIRI
wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu kushoto akiteta
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ziara hiyo |
Ummy alitoa agizo
hilo wakati wa ziara yake katika Jiji la Tanga kubwa ni kutokana na malalamiko
yanayotoka kwenye Jiji hilo kuhusu uchafuzi wa mazingira unaotokana na viwanda
vilivyopo vya kuzalisha saruji na chokaa.
Alisema kwamba suala la vifungashio alikwisha kutoa miezi mitatu ambapo mwezi Aprili mwaka huu ndio litakuwa limekwisha hivyo hategemei kuona baada ya kumalizika watu wataendelea kutumia vifungashio vya namna hiyo.
“Nisisitize suala la vifungashio nilitoa miezi mitatu mwezi wanne litakuwa limekwisha baada ya miezi mitatu kwisha tutatoa agizo la kuwaambia mkamatwe kwa yeyote ambaye anatumia vifungashio maana mifuko ya plastic imerudi kwa kigezo cha vifungashio”Alisema Waziri Ummy.
Aidha alisema kwamba hivi sasa unaona watu wameweka karoti wamezifunga kwenye mifuko kwamba wamerudisha mifuko ya plastic kwa kigezo cha vifungashio hivyo endele kuzibidi mifuko hiyo.
“Lakini ikiisha miezi mitatu niliyoitoa mtakayemkuta anaendelea kutumia mifuko ya plastic endeleeni kuchukua hatua stahiki dhidi yao “Alisema .
Hata hivyo Waziri Ummy alizitaka Halmashauri ziandae mpango kazi wa Mazingira ambao utakuwa na tija kubwa katika kusimamia na utekelezaji wa kazi hizo kwenye maeneo yao.
Alisema mpango huo lazima utengewe bajeti kwa sababu ni suala muhimu kama yalivyo masuala mengine ambayo yamekuwa yakifanyiwa hivyo katika maeneo husika.
“Pia tuhakikishe Halamshauri
zote zinaweka vipaumbele na bajeti ya kutekeleza shughuli za utunzaji na
uhifadhi mazingira lakini pia suala la uteuzi wa maafisa mazingira kwenye
mamlaka ya serikali za mitaa waendelee nalo”Alisema
Waziri Ummy Ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga alisema lakini changamoto zilizopo bado hakuna
mfumo mzuri wa ngazi ya halmashauri ya Usimamizi wa shughuli za Mazingira.
Kutokana na uwepo wa changamoto hiyo Waziri Ummy alimuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Kukaa na Katibu Mkuu Tamisemi ili kutengeneza mfumo mzuri .
Alisema kwa sababu
wanaweze kuwa wanapiga kelele mkoani lakini kama Halmashauri hazitakuwa na
mfumo nzuri wa kusimamia shughuli za mazingira hataweza kupata hayo matokeo
ambayo wameyapata ili tufanikishe lazima warekebishe muundo kwenye ngazi ya
Halamshauri za Serikali za Mitaa.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Afisa Mazingira Mkoa wa Tanga Thimotheo Sosiya alisema mkoa huu unatekeleza kampeni ya mazingira kwa pamoja kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na imeleta mafanikio makubwa kwenye kutkomeza uchafuzi maeneo korofi na mazingira.
Aisema lakini katika suala hilo changamoto kubwa ni uwezo mdogo wa Halmashauri kuondosha taka ngumu ikiwemo mwitiko mdogo wananchi kufanya usafi kwa hiari huku akieleza mkoa umejipanga.
Alisema kujipanga huko ni kuunda vikosi kazi kwenye Halmashauri ambavyo vitakuwa na kazi ya kusimamia mazingira na kwamba wanaotupa taka sasa wawepo watu ambao wanakuwa tayari kuwakamata na kuwapiga faini.
Social Plugin