Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum (kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha jezi kwa ajili ya shule katika kata ya Mwendakulima.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Azan Logistics imetoa msaada wa vitu vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7 ikiwa ni pamoja na bima za afya kwa wazee wasiojiweza kiuchumi na vifaa vya michezo kwa wanafunzi pamoja na posho za kujikimu kwa walimu wa kujitolea na kufunga umeme katika ofisi ya kata ya Mwendakulima Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa Jumatano Machi 17, 2021 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha katika ofisi ya Afisa Mtendaji wa kata ya Mwendakulima Manispaa ya Kahama.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum amesema Kampuni yake iliguswa na maisha ya wazee hivyo kuamua kuwakatia bima za afya (CHF iliyoboreshwa) wazee 60 kutoka vijiji vya Mwendakulima, Chapulwa, Busalala na Mwime ambapo jumla ya wanufaika ni 360.
"Tumewakatia bima za afya wazee 15 wasiojiweza kiuchumi kutoka kila kijiji kwenye vijiji vinne na kutoa kadi zingine tano kwa wategemezi wa wazee hao hivyo kufanya idadi ya bima za afya tulizotoa kuwa 360 ambazo zitawarahisishia kupata huduma za afya zote zikiwa na thamani ya shilingi milioni 1.8", amesema Azan.
"Tumekabidhi pia vifaa vya michezo zikiwemo jezi na mipira katika shule za msingi nne ambazo ni Chapulwa, Iboja, Budushi na Busalala vyenye thamani ya shilingi milioni 3.8", ameongeza Azan.
Aidha amesema wametumia shilingi milioni 1.1 kufunga umeme katika ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Mwendakulima na kutoa shilingi laki nne kama motisha kwa walimu kata ya Mwendakulima na kuwapa posho walimu 6 wanaojitolea katika shule kiasi cha shilingi milioni 2.4 ikiwa ni shilingi laki moja kwa kila mwalimu kwa kipindi cha miezi minne.
Azan ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia makundi ya watu wenye uhitaji wakiwemo wazee.
Akipokea vifaa hivyo mkuu wa wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ameishukuru na kuipongeza Kampuni ya Azan Logistics kwa kuwajali wazee kwa kuwapatia bima za afya akieleza kuwa wazee wana thamani kubwa akibainisha kuwa kama kuna makosa yanafanywa na baadhi ya watu katika jamii ni kutotunza wazee.
"Tunakushuru sana Azan kwa uzalendo wako wa kusaidia wazee kwani wajibu wa kila mmoja wetu kutunza wazee hawa ambao kimsingi ni wazazi wetu. Naomba wadau wengine kuona muhimu wa kutunza wazee katika jamii", amesema Macha.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka wazee kukataa kulea watoto walioachwa na watoto wao 'vijana wao' wenye uwezo wa kulea wanaoishi katika mikoa mingine kwani wanawapa kazi wazee huku wao wakiishi maisha ya anasa wazee wakiteseka.
Aidha ameishukuru kampuni ya Azan kwa msaada wa vifaa vya michezo shuleni hali itakayochochea michezo kwa wanafunzi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistic Co. Ltd, Azan Said Salum akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha bima za afya kwa ajili ya wazee katika kata ya Mwendakulima Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha bima za afya zilizotolewa na Kampuni ya Azan Logistic Co. Ltd kwa ajili ya wazee katika kata ya Mwendakulima Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea bima za afya zilizotolewa na Kampuni ya Azan Logistic Co. Ltd kwa ajili ya wazee 60 katika kata ya Mwendakulima Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi mzee kadi ya bima ya afya kutoka Kampuni ya Azan Logistic Co. Ltd
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi mzee kadi ya bima ya afya kutoka Kampuni ya Azan Logistic Co. Ltd
Wazee wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum (kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha jezi kwa ajili ya shule katika kata ya Mwendakulima.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akiangalia moja ya jezi zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum (kulia) kwa ajili ya shule katika kata ya Mwendakulima.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum (kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha mipira kwa ajili ya shule katika kata ya Mwendakulima.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum (kulia) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha mipira kwa ajili ya shule katika kata ya Mwendakulima.
Muonekano wa sehemu ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd, Azan Said Salum kwa ajili ya shule katika kata ya Mwendakulima.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea bima za afya kwa wazee na vifaa vya michezo shuleni katika kata ya Mwendakulima Halmashauri ya Manispaa ya Kahama vilivyotolewa na Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azan Logistic Co. Ltd, Azan Said Salum akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha bima za afya kwa wazee na vifaa vya michezo shuleni katika kata ya Mwendakulima Halmashauri ya Manispaa ya Kahama
Diwani wa kata ya Mwendakulima Abdulrahman Hassan akizungumza wakati wa Kampuni ya Azan Logistics ikikabidhi vifaa vya michezo na bima za afya kwa wazee katika kata ya Mwendakulima.
Afisa Mtendaji wa Kata wa Mwendakulima Gilbert Sichundwe akisoma taarifa ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Kampuni ya Azan Logistics Co. Ltd
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin