Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWILI WA BIBI WA OBAMA WAZIKWA KENYA



Sarah Obama ambaye ni Bibi wa Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama, amezikwa jana Machi 30,2021 nyumbani kwake Kogelo, Siays nchini Kenya.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na watu 100 tu  kutokana na marufuku mpya iliyotangazwa ya kupambana na ugonjwa wa Corona.

Sarah Obama alifariki juzi akiwa na miaka 99 katika Hospitali ya Jaramogi Oginga, Rais Mstaafu Obama, hakuhudhuria mazishi hayo lakini aliwasilisha salamu zake za pole Jumatatu.

Ulinzi mkali uliimarishwa kwenye kijiji cha Nyangoma Kogelo ili kuzuia maelfu ya waombolezaji walikuwa wanataka kuhudhuria mazishi ya Bibi Sarah.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com