Picha : BENKI YA CRDB SHINYANGA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUKUTANA NA WANAWAKE WAFANYABIASHARA


Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akizungumza leo Machi 8, 2021 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki hiyo.
Keki maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB tawi la Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga imeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, 2021 kwa kukutana na wafanyakazi wa benki ya CRDB na wanawake wafanyabiashara wateja wa Benki ya CRDB wanaomiliki akaunti ya Malkia ‘CRDB Malkia’ wakiwakilisha wateja wengine lengo likiwa ni kuhamasisha wanawake kuwa viongozi katika kila eneo walipo.

Maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani yamefanyika katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Muuguzi mstaafu Asteria Joliga ambaye ni mteja wa muda mrefu wa Benki ya CRDB.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney amesema benki hiyo imeamua kukutana na wanawake wafanyabiashara wateja wa Benki ya CRDB wanaomiliki akaunti ya Malkia ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya wanawake wenye lengo la kuwekeza ili kutimiza ndoto zao za mafanikio katika Nyanja mbalimbali.

“Lengo la maadhimisho haya ya siku ya wanawake duniani katika benki yetu ni kuhamasisha wanawake kuwa viongozi katika kila eneo walipo mfano kwenye biashara awe kiongozi, kulea familia awe kiongozi. Kwa kufanya hivyo tutakuwa na dunia yenye usawa”,amesema Mneney.

Mneney amefafanua kuwa usawa unagubikwa sana na uwezo wa mtu kiuchumi na jamii imekuwa na utamaduni wa kuwaweka nyuma wanawake kiuchumi, kielimu na kiungozi hivyo endapo wanawake watainuka kiuchumi itakuwa rahisi sana kufikia dunia yenye usawa.

Hata hivyo Mneney amewaomba wanawake wenye umri wa miaka kuanzia miaka 18 kuwa ana akaunti ya Malkia akibainisha kuwa CRDB Malkia ni mpango maalumu kwa wanawake unaolenga kuwainua kiuchumi kupitia mikopo nafuu na riba nafuu.

Kwa upande wake, Mgeni Rasmi Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB amewahamasisha wanawake kujiunga na akaunti ya Malkia ‘CRDB Malkia’ ambapo kiwango cha chini cha kufungulia akaunti hiyo ni shilingi 5000/= tu, hakuna gharama za kila mwezi,muda wa chini wa mpango wa akiba ni miezi 12 na kwamba riba inahesabiwa na kulipwa kila mwezi katika amana ya mteja na unaweza kupata mkopo hadi wa shilingi milioni 50.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB Tawi la Shinyanga yameenda sanjari na zoezi la kukata keki, kugonga cheers na kunywa chai ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Machi 8 mwaka huu (2021) kidunia ni: Wanawake katika Uongozi: Fanikisha Usawa katika Dunia yenye COVID-19 na Dhima ya kitaifa ni “Wanawake Katika Uongozi: Chachu kufikia Dunia yenye Usawa".

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Machi 8, 2021 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki hiyo ambapo imekutana na wanawake wafanyabiashara wateja wa Benki ya CRDB wanaomiliki akaunti ya Malkia ‘CRDB Malkia’ wakiwakilisha wateja wengine lengo likiwa ni kuhamasisha wanawake kuwa viongozi katika kila eneo walipo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza leo Machi 8, 2021 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki hiyo ambapo imekutana na wanawake wafanyabiashara wateja wa Benki ya CRDB wanaomiliki akaunti ya Malkia ‘CRDB Malkia’ wakiwakilisha wateja wengine
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akizungumza leo Machi 8, 2021 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki hiyo ambapo imekutana na wanawake wafanyabiashara wateja wa Benki ya CRDB wanaomiliki akaunti ya Malkia ‘CRDB Malkia’ wakiwakilisha wateja wengine. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB akizungumza leo Machi 8, 2021 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB.
Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB akizungumza leo Machi 8, 2021 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB.
Meneja Biashara Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akiandaa keki wakati wa zoezi la kukata wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB.
Muonekano wa keki wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB.
Muonekano wa keki wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB.
Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB akikata keki wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui, kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB akimlisha keki Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui (kushoto) kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney.
Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB akimlisha keki Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga , Luther Mneney. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui.
Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB akimlisha keki Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi.
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Mwanahamisi Iddi (kulia) akimlisha keki Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB. 
Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB akimlisha keki mteja wa benki ya CRDB
Zoezi la kula keki likiendelea
Mteja wa Benki ya CRDB akifungua shampeni
Zoezi la kugonga cheers likiendelea
Cheers!
Cheers!
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga. Luther Mneney akimkabidhi zawadi Mgeni rasmi Bi. Esteria Joliga ambaye ni Muuguzi Mstaafu na mteja wa Benki ya CRDB wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui.
Wanawake wafanyabiashara wanaomiliki akaunti ya Malkia wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wateja wa benki ya CRDB wakicheza muziki
Shamra shamra zikiendelea katika benki ya CRDB tawi la Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui  na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia) wakionesha makeke ya kucheza muziki wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake katika benki ya CRDB
MC Mama Sabuni (wa pili kushoto) ambaye ni mteja wa benki ya CRDB akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB
Mgeni rasmi Esteria Joliga akichukua vitafunwa na chai wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika benki ya CRDB
Zoezi la kuchukua chai/vitafunwa likiendelea
Uchukuaji chai/vitafunwa ukiendelea
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye foleni ya kuchukua chai
Wateja wa benki ya CRDB wakinywa chai
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Luther Mneney akinywa chai na wateja wa benki ya CRDB
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakichukua chai na juisi
Wateja wa benki ya CRDB wakiwa na fomu za kujiunga na akaunti ya Malkia
Picha ya pamoja mgeni rasmi,wafanyakazi wa benki ya CRDB na wateja wa benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu
Mgeni rasmi akipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa benki ya CRDB 
Mgeni rasmi akipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wanawake wa benki ya CRDB
Mgeni rasmi akipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wanaume wa benki ya CRDB.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post