Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kulia) akiwa ameshikilia boksi la chaki alipotembelea Kiwanda cha Chaki 'Shinyanga Standard Chalk' na kujionea kazi inayofanyika katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifuatiwa na mwenyekiti wa kiwanda hicho, Hashim Issa
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akisaini kitabu cha wageni ndani ya stoo ya Kiwanda cha Chaki 'Shinyanga Standard Chalk' wakati akijionea kazi inayofanyika katika kiwanda hicho
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kushoto) akiangalia chaki zilizotolewa kwenye mtambo muda mfupi baada ya kutengenezwa katika Kiwanda cha Chaki 'Shinyanga Standard Chalk'
Muonekano wa maboksi ya chaki za Kiwanda cha Shinyanga Standard Chalk
****
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba ametembelea Kiwanda cha Chaki 'Shinyanga Standard Chalk' na kujionea kazi inayofanyika katika kiwanda hicho kinachoendeshwa na vijana kilichopo katika Mtaa wa Miti Mirefu Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika kiwanda hicho Machi 2,2021, Mhe. Kirumba
aliwapongeza viongozi wa serikali wilaya ya Shinyanga kwa kuendelea kuwapigania vijana katika kupata fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uanzishwaji wa kiwanda hicho cha kwanza cha kutengeneza chaki katika mkoa wa Shinyanga.
Mhe. Kirumba aliwapongeza vijana hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kiwanda hicho, Hashim Issa kwa uthubutu wao kuanzisha kiwanda pamoja na changamoto zote wanazopitia ikiwemo ya kukosa soko la uhakika waendelee kutengeneza chaki nzuri na zenye kiwango.
Katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na vijana hao, mbunge Santiel Kirumba aliwachangia kiasi cha shilingi 250,000/= kama mchango wake katika kuchochea shughuli za kiwanda.
Soma pia: