Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KASHI SALULA ACHAGULIWA KUWA MJUMBE MWAKILISHI KUTOKA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA SHINYANGA KWENDA UVCCM


Kashi Salula akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua kuwa mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) 

Na Suzy Luhende - Shinyanga
Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga imefanya uchaguzi mdogo wa kumchagua mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM)  na kumchagua Kashi Salula kuchukua nafasi ya aliyekuwa mjumbe wa nafasi hiyo Asha Mwandu  kupewa adhabu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kosa la kimaadili.

Uchaguzi huo umefanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga uliopo mjini Shinyanga, ambapo Kashi Salula amechaguliwa mjumbe mwakilishi kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo.

Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa uchaguzi huo Mwalimu Patrick Kija amesema wapiga kura walikuwa 15 mgombea alikuwa mmoja, ambapo kura zilikuwa zinapigwa za hapana na ndiyo, hakuna iliyoharibika kura za hapana zilikuwa 2 na kura za ndiyo zilikuwa 13 hivyo Kashi Salula ameshinda kwa kura 13.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salu amesema baada ya nafasi hiyo kukosa mwakilishi walitoa matangazo kwa siku saba ambapo amepatikana mgombea mmoja ambaye ndiye Kashi Salula.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga, Alhaj Salum Abdalah Simba amesema kwa mujibu wa utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilitoa nafasi ya kujaza nafasi zilizo wazi kuanzia ngazi ya wazazi na ndani ya Chama Cha Mapinduzi, hivyo wametimiza agizo walilopewa wamepata mwakilishi wa nafasi hiyo.

Simba amesema mjumbe aliyetoka kwenye nafasi hiyo alikuwa anawakilisha Jumuiya ya Wazazi kwenda Vijana lakini baada ya kufanya makosa ya kimaadili ndiyo maana kimefanyika kikao cha dharula cha Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuziba nafasi yake.

"Nawashukuru sana wajumbe kwa kuitikia na kuthamini uchaguzi, leo tumejaza nafasi ya mapungufu yaliyokuwepo hivyo tunakukaribisha sana kwenye Jumuiya hii ambayo haina ubaguzi, sisi tunachukua wote kutoka umoja wa vijana UVCCM na Umoja wa wanawake UWT, wajumbe nawaomba tumpokee kwa mikono miwili Kashi Salula  tumsaidie na atusaidie", amesema Simba.

Kwa upande wake mjumbe mwakilishi aliyechaguliwa Kashi Salula amesema anawashukuru kwa kumchagua  kwani ameiomba nafasi hiyo ili aweze kushirikiana na viongozi, wajumbe kwa ajili ya kukitumikia Chama Cha Mapinduzi CCM kwa uaminifu wote.

"Nawashukuru sana kwa kunichagua kwani tutafanya kazi kwa uaminifu ili kuendelea kukijenga chama chetu, na kuhakikisha kinasonga mbele na kuendelea kuchukua ushindi, na tutasimama kidete kwa kushirikiana na Rais wetu Mpendwa Dk. John Pombe Magufuli na kutimiza maono yake ya kulijenga Taifa la Tanzania",amesema Kashi.
Kashi Salula akiomba kura kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga wakati wa  uchaguzi mdogo wa kumchagua mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) .Picha na Suzy Luhende
Kashi Salula akiomba kura kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga wakati wa  uchaguzi mdogo wa kumchagua mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) 
Mwalimu Patrick Kija ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo wa kumchagua mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) akizungumza
Kashi Salula akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua kuwa mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) 
Kashi salula akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua kuwa mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) 
Kashi salula akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua kuwa mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) 
Kashi Salula akiwa na vingozi wa kamati ya utekelezaji baada ya kuchaguliwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga, Alhaj Salum Abdalah Simba akizungumza baada ya uchaguzi mdogo kumchagua kuwa mjumbe Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kwenda Jumuiya  vijana CCM Mkoa wa Shinyanga (UVCCM) kuisha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga, Alhaj Salum Abdalah Simba  akizungumza baada ya uchaguzi huo kuisha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga, Alhaj Salum Abdalah Simba  akizungumza baada ya uchaguzi huo kuisha
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga, Alhaj Salum Abdalah Simba  akizungumza baada ya uchaguzi huo kuisha
Katibu wa Jumuia ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga  Masanja Salula akizungumza wakati wa uchaguzi huo
Kashi Salula akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga
Kashi Salula akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga
Kashi Salula akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake waliomsindikiza kwenye uchaguzi
Kashi Salula akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wake waliomsindikiza kwenye uchaguzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com