Askofu wa Kanisa la The International Evangelical Assemblies Of God –Tanzania (IEAGT) lililopo katika kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga David Mabushi akiongoza ibada ya Jumapili leo Machi 21,2021 akiliombea taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kuongoza kwa amani na utulivu
Askofu wa Kanisa la The International Evangelical Assemblies Of God –Tanzania (IEAGT) lililopo katika kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga David Mabushi akiongoza ibada ya Jumapili leo Machi 21,2021 akiliombea taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili aweze kuongoza kwa amani na utulivu
Waumini wa Kanisa la The International Evangelical Assemblies Of God –Tanzania (IEAGT) lililopo katika kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga wakiombea Taifa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuongoza nchi kwa amani na utulivu
Waumini wa Kanisa la The International Evangelical Assemblies Of God –Tanzania (IEAGT) lililopo katika kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga wakiombea Taifa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuongoza nchi kwa amani na utulivu
**
Na Suzy Luhende - Shinyanga.
Askofu wa Kanisa la The International Evangelical Assemblies Of God –Tanzania (IEAGT) lililopo katika kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga David Mabushi amewataka Watanzania wote kushikamana na kuondoa itikadi za kisiasa, kidini na kikabila badala yake waungane washirikiane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kufanya kazi za kimaendeleo ya nchi ya Tanzania.
Hayo ameyasema leo Machi 21,2021 wakati akihubiri neno la Mungu katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa hilo mbapo alisema Watanzania wanatakiwa kuondoa tofauti zao katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli badala yake washikamane katika kulijenga taifa la Tanzania.
Askofu Mabushi amesema kuondokewa na Rais Magufuli ni pigo kubwa kwa Watanzania na Afrika kwani alifanya mambo makubwa na alikuwa na maono makubwa ya kuweza kuiendeleza nchi, hivyo watanzania wote wanatakiwa kuwa watulivu na kuonyesha ushirikiano kwa kiongozi aliyeteuliwa kuongoza Samia Suluhu ili aendeleze maono yaliyoachwa na Hayati Rais Magufuli.
"Sasa ni wakati wa kuweka pembeni tofauti zetu za chama kwa sababu nchi imeguswa pakubwa, jambo la ajabu mnakuta mtu anaweka itikadi kwamba huyu siwezi kumzika kwa sababu ni wa chama furani, hapana tusifanye hivyo tusitangulize itikadi zetu, Magufuli amefanya mambo makubwa sana katika nchi hii ambayo wanafaidika watu wote na vyama vyote vilivyomo nchini hapa si kwa ajili ya familia yake", amesema Askofu Mabushi.
"Kwa yale aliyoyafanya hatuna cha kumlipa, kanisa na nchi kwa ujumla tumepata pengo kubwa tuendekee kumuenzi, lakini tumshukuru tu Mungu ametuletea mtu mzuri ambaye ataongoza vizuri, tumuombee Rais Samia aliyeshika usukani kwa wakati huu afanye mema kwa sababu amemuweka kwa wakati, sisi hatukujua kama mama huyu atakuwa Rais wetu, lakini yeye Mungu alijua tusimame naye kwa umoja,"amesema Mabushi.
Askofu Mabushi pia ameungana na waumini wa kanisa hilo katika kuliombea Taifa na kumuombea Mjane wa Dk. Magufuli, Janeth Magufuli kwa msiba huo pia kwa pamoja kanisa hilo lilifanya maombi ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan aweze kuongoza nchi kwa amani na utulivu.
Mabushi amesoma neno la Mungu kutoka Mwanzo 25: 8-9 ambayo inamzungumzia Ibrahimu aliyekuwa kiongozi alipokufa alikuja kiongozi mwingine Ishimail ambaye walishirikiana nae vizuri, hivyo na watanzania waondoe hofu kwa sababu neno la Mungu linasema watainuka viongozi wengi wakiwemo wakiume na wakike hivyo neno la Mungu limetimia.
"Ninampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza nchi ya Tanzania kwani wanawake wana umuhimu mkubwa sana katika Taifa na katika familia, mwanamke ni daktari na tumepata mama wa kuongoza nchi yetu tukisimama nae tutafanya maendeleo tusimchokoze chokoze tukimpa nafasi atatuhudumia vizuri", amesema Askofu Mabushi.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo Albano Mazimo, Zefania Robert na Mercyline Paul wamesema watanzania wakiondoa tofauti na kuwa wamoja Tanzania itasimama, kinachotakiwa ni kumuombea kiongozi mpya aendeleze yaliyoachwa.
Social Plugin