Dkt. John Pombe Magufuli
Kampuni ya Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ,Malaika Cleaning Service (Macleans) ya jijini Dar es salaam imeungana na Watanzania kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Macleans , Alloysius Madata amesema Kampuni yake imepokea kwa masikitiko makubwa sana msiba huu wa kitaifa wa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Magufuli kwani alikuwa chachu thabiti ya maendeleo endelevu ya taifa la Tanzania.
Madata amesema Dkt. Magufuli, alikuwa mtetezi wa wanyonge na alionyesha kuwajali na kuwapenda na ndiyo chanzo cha wajasiriamali wengi kuinuka kiuchumi na maisha yao ya kila siku.
Aidha amesema kampuni yake itaendelea kumuenzi na kuyaenzi mambo yote muhimu ikiwa pamoja na maendeleo aliyotuletea katika taifa
Amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushika usukani wa kuliongoza Taifa na kwamba anamuombea kwa Mungu aweze kutekeleza vyema majukumu yake.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE,AAMEN!!
Social Plugin