SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA VIONGOZI MBALIMBALI KUFUATIA KIFO CHA RAIS MAGUFULI

 

Rais Magufuli enzi za uhai wake

 Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa pole kwa watanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kupitia mtandao wa Twitter ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo hicho:

Ruka Twitter ujumbe, 1

 Kiongozi wa upinzani wa chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania Bw. Zitto Kabwe amesema pia amezungumza kwa njia ya simu na Rais -Mteule wa Tanzania Samia Suluhu na kumtolea salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli:

Ruka Twitter ujumbe, 2

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ametoa salamu za pole kwa taifa la Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo Behgjet Pacolli ametoa salamu kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 majira ya saa 12:00 Jioni.

Mama Samia amesema Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. 

Mtandao huu wa Malunde 1 blog Malunde 1 blog  pia umepokea kwa masikitiko  makubwa taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na unaungana na Watanzania wote kwenye maombelezo ya  kitaifa ya siku 14 kama yalivyotangazwa na serikali. 

Mungu ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Rais wetu Mpendwa Dk. John Pombe Magufuli. Amina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post