Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa pole kwa watanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
I'm sorry to hear that @MagufuliJP, President of Tanzania, has passed away. My thoughts are with his loved ones and the people of Tanzania.
— Boris Johnson (@BorisJohnson) March 17, 2021
Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kupitia mtandao wa Twitter ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo hicho:
Kwa masikitiko makubwa tarehe 17th March 2021, saa 12 jioni tumempoteza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.— Dr Hussein Ali Mwinyi (@DrHmwinyi) March 17, 2021
Kiongozi wa upinzani wa chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania Bw. Zitto Kabwe amesema pia amezungumza kwa njia ya simu na Rais -Mteule wa Tanzania Samia Suluhu na kumtolea salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli:
I have just spoken over the phone with President-Elect of Tanzania @SuluhuSamia and offer condolences following the death of President @MagufuliJP as officially announced today by the Vice President.
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) March 17, 2021
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ametoa salamu za pole kwa taifa la Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Le Chef de l'État, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo a appris avec une grande tristesse la disparition de son homologue et frère, M. John Magufuli, Président de la Tanzanie.— Présidence RDC (@Presidence_RDC) March 17, 2021
Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali na taifa la Somalia, ningependa kuwasilisha rambi rambi zetu kwa Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania kwa kumpoteza Kiongozi Rais John Magufuli. Tunalitakia taifa Zima na Serikali subra na utulivu katika kipindi hiki cha maombi na maombolezo. pic.twitter.com/cQz3rALaPt
— Mohamed Farmaajo (@M_Farmaajo) March 17, 2021
Rais wa Venezuela Nicolás Maduro ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
Expresamos nuestras sentidas condolencias al Pueblo de Tanzania por la sensible pérdida física de su Presidente, John Pombe Joseph Magufuli. Un gran abrazo fraterno y toda la solidaridad a sus familiares, amigos y hermanos de la Madre África. pic.twitter.com/jf90XYXKoy
— Nicolás Maduro (@NicolasMaduro) March 18, 2021
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo Behgjet Pacolli ametoa salamu kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
#Venezuela expresses its consternation for the death of the President of the United Republic of #Tanzania, Honorable John Pombe Joseph Magufuli. Our condolences and solidarity to his family, his government and the brother Tanzanian people. May he rest in peace! pic.twitter.com/Pu4tAWzuXi
— Jorge Arreaza M (@jaarreaza) March 17, 2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 majira ya saa 12:00 Jioni.
Mama Samia amesema Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mtandao huu wa Malunde 1 blog Malunde 1 blog pia umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na unaungana na Watanzania wote kwenye maombelezo ya kitaifa ya siku 14 kama yalivyotangazwa na serikali.
Mungu ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Rais wetu Mpendwa Dk. John Pombe Magufuli. Amina.
Social Plugin