UTARATIBU WA KUAGA MWILI WA MAGUFULI WABADILISHWA....SASA WANANCHI HAWATAPITA MBELE YA JENEZA
Monday, March 22, 2021
Viongozi mbalimbali wameanza kuingia katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli huku utaratibu ukibadilishwa.
Utaratibu wa kuaga mwili wa Magufuli umebadilishwa ambapo sasa wananchi hawatapita mbele ya jeneza lenye mwili wake badala yake walio ndani ya uwanja huo wataaga mwili ukiwa kwenye gari na utazungushwa uwanjani hapo mara tano ukiwa katika gari maalum.
Social Plugin