Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, leo Machi 26, 2021, umepumzishwa katika nyumba yake ya milele kwenye makaburi ya familia yaliyopo Chato mkoani Geita.
Shughuli ya mazishi hayo imeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mke wa marehemu Mama Janeth Magufuli, marais wastaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.
Mbali na hao shughuli hiyo pia imeshuhudiwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanafamilia, Mawaziri, Makatibu Wakuu, wasanii pamoja na baadhi ya wakazi wa Chato na maeneo jirani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Taifa wakati wa mazishi ya mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kijijini Chato mkoa wa Geita Ijumaa Machi 26, 2021
Pakua / Download App ya Malunde 1 blog Tuwe tunakutumia taarifa zote moja kwa moja kwenye simu yako bure kabisa
Social Plugin