Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIKAGUA GWARIDE LA JWTZ LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano kipindi cha pili katika hafla iliyofanyika leo tarehe Machi 19, 2021 katika Ikulu ya Magogoni Mkoa wa Dar es Salaam. Ikiwa Hafla iliyofanyika kwa majonzi kwa sababu ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mnzena Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan akipokea salamu za kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo Machi 19, 2021.
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Machi 19, 2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com