Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : RAIS SAMIA AMPENDEKEZA DKT. PHILIP MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS


Dkt. Philip Mpango.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jina la Dkt. Mpango limesomwa bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa kiongozi mkuu huyo wa nchi.

 Spika Ndugai ameanza kusoma nyaraka hiyo ya Mhe. Rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina ambapo
baada ya kusoma jina wabunge walishangilia kwa nguvu.

Wakati hayo yakiendelea Dkt. Mpango alionekana kushikwa na butwaa huku wabunge wakinyanyuka kwenye viti vyao na kumfuata kumpongeza kisha Dkt. Mpango akasimama kuzungumza akishukuru kwa pendekezo hilo huku akielezea pia historia yake.

Kinachofuata sasa ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuthibitisha jina lake katika kikao cha bunge kinachoendelea muda huu jijini Dodoma na utaratibu wa kupiga kura ili kuthibitisha jina hilo utafanyika bungeni leo.

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com