Mabao ya Luis Miquissone dakika ya 18, Mohamed Hussein 'Tshabalala' dakika ya 39 na Chris Mugalu dakika ya 50 yameipa Simba SC ushindi wa 3-0 dhidi ya Al Merreikh ya Sudan katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika leo Machi 16,2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo Simba SC inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.
Simba inatazamiwa kushuka tena dimbani tarehe 2 mwezi Aprili 2021 kukipiga na AS Vita kwenye dimba la Mkapa huku ikitafuta alama pekee kujihakikishia kufuzua hatua ya robo fainali kabla ya kumaliza mchezo wa mwisho wa makundi kwa kucheza na Al Ahly tarehe 9 April 2021 nchini Misri.
Social Plugin