Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TGNP, UNFPA WAENDESHA MDAHALO KWA WANAUME NA WATU MAARUFU KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA MSALALA

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikina na UNFPA wameendesha mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya na wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.

Mdahalo huo umefanyika Machi 25,2021 kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia na jamii ipate nafasi ya kuweka mikakati ya kuzuia ukatili wa kijinsia na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba amesema mdahalo huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na TGNP na UNFPA katika kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya wilaya ya Msalala.

Amesema TGNP inaendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) ikiwa imejikita zaidi katika kutokomeza mila na desturi zinazochochea ukatili wa kijinsia.

“Tumewakutanisha pamoja watu maarufu katika kata ya Lunguya wakiwemo viongozi wa jeshi la jadi sungusungu,wazee wa mila (Wakango),viongozi wa dini,siasa,wafanyabiashara, wakulima, maafisa watendaji wa vitongoji na vijiji,wahudumu wa afya ngazi ya jamii na vituo vya taarifa na maarifa. Kwa upande wa kata ya Shilela tumefanya mdahalo na kundi la wanaume wenye miaka kuanzia 18 hadi 60”,amefafanua Temba.

“Kupitia midahalo hii tunaamini kabisa italeta mabadiliko makubwa katika kutokomeza ukatili wa kijinsia lakini pia kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa zanahati ,vyoo na mabweni katika shule”,amesema Temba.

Wakizungumza wakati wa midahalo hiyo, washiriki wamesema bado katika kata hizo kuna changamoto ya mimba na ndoa za utotoni, vipigo kwa wanawake, wanawake kutomiliki ardhi na kutoshirikishwa katika maamuzi, matumizi ya lugha mbaya (matusi) kwa wacheza ngoma ya ukango na wazazi kutokuwa karibu na watoto wao.

Wamesema hali duni ya kiuchumi na utandawazi na kukosekana kwa ulinzi kwa watoto vinachochea matukio ya ukatili wa kijinsia.

Kufuatia midahalo hiyo,wametengeneza mpango kazi kuhusu namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika maeneo yao huku wakipendekeza serikali za vijiji ziunde sheria ndogo kwa ajili ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Msalala, Neema Katengesya amewataka washiriki wa mdahalo huo kuwa mstari wa mbele kupiga vita na kuwa tayari kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia.

“Tutaondoka katika hali endapo kila mmoja atakuwa tayari kubadilika na kuwa na mitazamo chanya kuhusu wanawake na watoto kama vile kutokubali watoto waolewe katika umri mdogo, wazee wa mila maarufu ‘Wakango’ kuepuka kuvaa nguo nusu uchi na kutumia lugha chafu wakati wa sherehe wanazoandaa kuwafanyia matambiko watoto mapacha”,amesema.

Aidha amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao na kuwa wawazi kuwaeleza kuhusu vitendo ambavyo vinaweza kukatisha ndoto ikiwemo kufanya ngono katika umri mdogo.

Pia amepiga marufuku wazazi kupeleka watoto wao wa kike kwa waganga wa kienyeji wakaoshwe dawa za mvuto ‘samba’ ili kuwavutia wanaume badala yake wawapeleke watoto shule.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Msalala Neema Katengesya akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Diwani wa kata ya Lunguya Mhe. Benedict Mussa akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia

Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia

Watu maarufu kata ya Lunguya wakiendelea na mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia chini ya mti wa mwembe katika Senta ya Lunguya
Mshauri Jamii na Mtafiti kutoka TGNP, Catherine Mzurikwao akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mdahalo unaendelea
Mdahalo ukiendelea
Watu Maarufu kutoka Lunguya wakiwa kwenye mdahalo
Mganga wa Kienyeji Masanja Tabo akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mzee maarufu Helena Busobe akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mwana kituo cha taarifa na maarifa Lunguya, Gaudensia Madaha akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo ukiendelea
Kiongozi wa dini akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo ukiendelea
Mdahalo ukiendelea
Mdahalo ukiendelea
Kiongozi wa dini akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mzee Joseph Sonda akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa kata ya Lunguya Loyce Kabanza akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo ukiendelea
Mkazi wa Lunguya akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mdahalo unaendelea
Mshauri Jamii na Mtafiti kutoka TGNP, Catherine Mzurikwao akifuatilia mjadala wakati wa kutengeneza mpango kazi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akijadili jambo na wazee wa mila ambao ni Wacheza ngoma ya mapacha 'Ukango'
Washiriki wa mdahalo wakitengeneza mpango kazi wa namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia
Washiriki wa mdahalo wakitengeneza mpango kazi wa namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 60 kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mshauri Jamii na Mtafiti kutoka TGNP, Catherine Mzurikwao akizungumza wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Wakazi wa kata ya Shilela wakionesha mchezo wa Igizo wakati Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mkazi wa Shilela, Msigwa Pastor akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Mkazi wa Shilela Jumanne John akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Wanakikundi cha Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela wakifuatilia matukio wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mkazi wa Shilela Jumanne Masaga akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Mkazi wa Shilela Andrew Mayala akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Wakazi wa Shilela wakijadili mpango kazi wa namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala

Wakazi wa Shilela wakijadili mpango kazi wa namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com