Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart' Scholastika Kavela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart' Scholastika Kavela amesema wana imani kubwa ya utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan na kuwataka Watanzania kumuunga mkono kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake wa kiti hicho Hayati Dk. John Magufuli.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kevala alisema hana mashaka na utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni mchapakazi wa kweli na kwamba yeye na kampuni yake wataendelea kusimama pamoja naye wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake.
"Kwanza kabisa tunampa pole kwa msiba wa mtangulizi wake sote tukiamini kuwa hayo yote ni mapenzi ya Mungu ...nasi tumepokea kwa masikitiko kama ilivyo kwa watanzania wote na ulimwengu kwa ujumla" alisema Kevela
Alisema watanzania kwa wanaamini chini ya uongozi wa Mama Samia Tanzania itazidi kupiga hatua za kimaendeleo huku akiwataka wasaidizi wake wa ngazi zote kumuunga mkono.
Alisema endapo watendaji hao waliopo chini yake watatimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ni wazi watakuwa nguzo nzuri kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza malengo yake kwa Taifa hili.
Alisema nyota njema huonekana tangu asubuhi na kwamba hata utendaji wa kazi wa Rais ulionekana tangu akiwa na nyadhifa zingine ndani ya Serikali tofauti na hiyo ya ngazi ya juu aliyonayo hivi sasa.
"Rais alishajipambanua katika utawala ndani miaka mingi, ameshashika nafasi za juu katika Serikali ikiwemo ya Makamu wa Rais, Waziri katika Serikali ya awamu ya nne na hata Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, uzoefu wake unamtosha kuliongoza Taifa hili", alisisitiza Kevela.
Alisema hatua ya yeye kuwa Rais wa Taifa hili kwa kiasi kikubwa kumeweza kuionyesha Dunia na ulimwengu mzima kuwa Tanzania ni nchi isiyokumbatia masuala ya mfumo dume unaotoa fursa kwa jinsia moja kushika nyadhifa ya juu ya uongozi.
Alisema hatua hiyo pamoja na kupokelewa vyema na wananchi wote zaidi kumewaheshimisha wanawake nchini na dunia nzima na kumuona kama mfano kwao katika jitihada za kujiletea maendeleo.
"Tunamuombea kwa Mungu aweze kumpa ulinzi wa kutosha na afya njema wakati wote ili aweze kutekeleza ipasavyo majukumu ya kututumikia wananchi wake", alisema Kevela.
Alisema Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ipo katika mikono salama na zaidi akawaoamba wananchi kumuunga mkono kwa kuchapa kazi bila kuchoka ili kulisukuma mbele Taifa la Tanzania.
Social Plugin