Mafunzo kwa Vitendo yakiendelea katika uwanja wa mpira wa Miguu wa shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.
Na Josephine Charles - Malunde1 blog
Bonanza la Mpira wa
Miguu kwa watoto wadogo kuanzia miaka 4 mpaka 12 yaani FIFA Grass Roots
linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia
iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga Jumamosi ya tarehe
20 mwezi March 2021.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Grass Roots Mkoa wa Shinyanga Fr. Joachim Michael pamoja na Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Daniel Mbilinyi wakati wa mahojiano maalum na Malunde1 blog na kusema kwamba bonanza hilo litaanza majira ya saa mbili asubuhi.
Wamesema Bonanza hilo ni mahususi kwa watoto wa shule za msingi zinazopatikana katika kata zinazozunguka eneo la Don Bosco zikiwemo kata za Didia,Puni,Nyida,ILola,Imesela na Itwangi,na hiyo ni baada ya kutolewa kwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Waalimu wa Shule za Msingi na Sekondari Takriban 22 kutoka kata hizo ambayo yalifanyika Jumamosi ya 13 March 2021 katika Shule ya Sekondari Don Bosco.
Bonanza hilo
litakalofanyika Jumamosi Machi, 20 2021 ni mwendelezo wa Mafunzo yaliyotolewa
siku ya Jumamosi ya tarehe 13 March 2021 ambalo litahusisha wasatani wa watoto
120 wakike nawa kiume wa Darasa la Kwanza,Pili,Tatu,Nne,Tano,Sita,Saba na
baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza.
Aidha Lengo ni kuwafundisha watoto wadogo wenye umri kuanzia miaka 4 hadi 12 pamoja na kuwajengea msingi wa soka tangu wakiwa wadogo katika Mkoa wa Shinyanga pia kuona namna Waalimu waliopatiwa mafunzo wanavyoweza kuwasimamia na kufundisha watoto hao wadogo wakike nawa kiume.
Tazama Picha hapa chini.
Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Daniel Mbilinyi ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Nyihogo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama akitoa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Waalimu wa Shule za Msingi na Sekondari kutoka kata za Didia,Puni,Nyida,ILola,Imesela na Itwangi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia-Shinyanga.Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Daniel Mbilinyi ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Nyihogo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama akitoa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Waalimu wa Shule za Msingi na Sekondari kutoka kata za Didia,Puni,Nyida,ILola,Imesela na Itwangi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia.
Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Daniel Mbilinyi ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Nyihogo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama akiendelea kutoa Mafunzo kwa Vitendo.
Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Daniel Mbilinyi ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Nyihogo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama akiendelea kutoa Mafunzo kwa Vitendo.
Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Daniel Mbilinyi ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Nyihogo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama akiendelea kutoa Mafunzo kwa Vitendo.
Baadhi ya Waalimu wa Michezo waliohudhuria Mafunzo,wakionesha kwa vitendo yale waliyofundishwa na Mkufunzi wa Mafunzo hayo Mwalimu Daniel Mbilinyi ambaye pia ni Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga ili nao wakawafundishe Wanafunzi wao.
Baadhi ya Waalimu wa Michezo na Wanafunzi waliohudhuria Mafunzo,wakionesha kwa vitendo yale waliyofundishwa na Mkufunzi wa Mafunzo hayo Mwalimu Daniel Mbilinyi ambaye pia ni Meneja Ufundi TFF Grass Roots Mkoa wa Shinyanga ili nao wakawafundishe Wanafunzi wao.