FOLENI NDEFU KATIKA MFEREJI WA SUEZ MISRI BAADA YA MELI MOJA KUFUNGA NJIA


 Baada ya meli moja Kubwa kukosea njia na kukwama katika Mfereji wa Suez huko Misri na kushindwa hadi hivi sasa kukwamuliwa ilipokwama, sasa hivi kuna zaidi ya meli 321 zimepanga foleni zikisubiri kupita katika mfereji huo.

Kila siku karibu meli 50 zinapita katika Mfereji wa Suez. Mfereji huo ulianza kujengwa mwaka 1859 na ulimaliza kujengwa mwaka 1869. Unaliunganisha bara la Asia na bara la Ulaya kupitia Bahari ya Meditarenean na Bahari Nyekundu au Bahari ya Shamu.

Mfereji wa Suez ndiyo njia ya mkato zaidi ya kuelekea Ulaya kutokea Asia. Takriban asilimia 7 ya uchukuzi wa baharini wa kibiashara unafanyika kupitia Mfereji wa Suez huko Misri ambao ni sehemu muhimu sana ya pato la kigeni la nchi hiyo.

Meli kubwa la Ever Green lenye uzito wa karibu tano laki mbili na 20 elfu na urefu wa mita 400, Jumanne iliyopita meli hilo lilipata matatizo ya kiufundi, likafunga njia. Meli hilo lilikuwa linatokea China na lilikuwa linaelekea Rotterdam na mmiliki wake ni shirika moja la Taiwan.


Meli nyingi zimelazimika kugeuza njia na kuelekea Bahari ya Hindi kwa ajili ya kulizunguka bara la Afrika kuelekea barani Ulaya, suala ambalo litaongeza muda wa wiki nzima zaidi hadi kufika zinakokusudia.

Bei ya mafuta nayo imepanda duniani kutokana na kushindwa meli hizo kupita katika Mfereji wa Suez.

 

Credit:Parstoday



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post