Picha : JIELONG HOLDINGS LTD, KANISA LA BAPTISTI WAKABIDHI MADAWATI SHULE ZA KIZUMBI..DC MBONEKO AAGIZA WATORO WAFUATILIWE

Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko meza 40,viti 40 na madawati 10 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amekabidhi madawati, meza na viti vyenye thamani ya shilingi milioni 3.5 yaliyotolewa na Kiwanda cha mafuta ya kula cha Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende kwa ajili ya shule ya msingi Kizumbi na shule ya Sekondari Kizumbi zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Mhe. Mboneko amepokea meza,viti na madawati kutoka kwa wadau Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende na kukabidhi kwa shule za msingi na sekondari Kizumbi leo Jumanne Machi 30,2021.

Mkuu huyo wa wilaya amekabidhi meza 40, viti 40 na madawati 10 kwa ajili ya shule ya Sekondari Kizumbi vyenye thamani ya shilingi Milioni 3.1 na madawati sita yenye thamani ya shilingi laki 4 kutoka Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu kwa ajili ya shule ya msingi Kizumbi.

Akizungumza, Mboneko ameishukuru Kampuni ya Jielong Holdings (T) LTD na Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu kwa mchango wao katika sekta ya elimu kwa kusaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa viti na meza pamoja na madawati katika shule ya msingi Kizumbi na shule ya sekondari Kizumbi.

“Tunawashukuru wadau wetu kwa kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutupatia meza,viti na madawati. Suala la kuboresha miundombinu ya shule ni la kila mtu,naomba wadau wengine,wawekezaji wengine waliopo ndani na nje ya wilaya ya Shinyanga wajitokeze kusaidia ili tumalize changamoto zilizopo katika shule mbalimbali ili watoto wetu wasome katika mazingira bora”,amesema Mboneko.

“Sisi serikali kazi yetu ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri, wazazi kuhimiza watoto waende shule na kuwapatia mahitaji muhimu nanyi wanafunzi kuhakikisha mnasoma kwa bidii na kuepuka vishawishi vinavyoweza kukatisha ndoto zenu ikiwemo kupata ujauzito mngali wanafunzi”,ameongeza Mboneko.

Mboneko ametumia fursa hiyo kuwapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwashukuru walimu watano wanaojitolea kufundisha katika shule ya sekondari Kizumbi.

Katika hatua nyingine amesema suala la utoro kwa wanafunzi halikubaliki hivyo amewaagiza walimu ,wazazi na viongozi wa idara ya elimu katika wilaya ya Shinyanga kufuatilia wanafunzi watoro warudishwe shuleni kuendelea na masomo.

Pia ametoa taarifa ya serikali kuleta fedha shilingi milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule ya  Sekondari Kizumbi na shilingi milioni 12.5  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa darasa katika shule ya msingi  Bugayambelele iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji amesema wamechangia viti,meza na madawati ili kushirikiana na serikali katika kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

Aidha amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu amesema wameamua kuchangia madawati katika shule ya msingi Kizumbi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akipokea na kukabidhi meza,viti na madawati kutoka kwa wadau Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende na kukabidhi kwa shule za msingi na sekondari Kizumbi leo Jumanne Machi 30,2021. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Doris Dario, kushoto ni Mkuu wa shule ya sekondari Kizumbi, Marco Msangwa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akipokea na kukabidhi meza,viti na madawati kutoka kwa wadau Jielong Holdings (T) LTD na Kanisa la Baptisti Nyanhende na kukabidhi kwa shule za msingi na sekondari Kizumbi leo Jumanne Machi 30,2021.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatunza meza,viti na madawati yaliyotolewa na wadau.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akizungumza wakati akikabidhi meza 40,viti 40 na madawati 10 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Mfanyakazi wa kiwanda hicho Bi. Khadija Yusuph akitafsiri lugha ya Kichina kwenda Kiswahili.
 Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Nyanhende, Renatus Kanunu akizungumza wakati akikabidhi madawati sita kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko meza 40 na viti 40 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko meza 40 na viti 40 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko madawati 10 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ,viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye meza 40 na viti 40 vilivyotolewa na Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kilichopo eneo la Nhelegani Mjini Shinyanga, Zhongjun Ji, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ,viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati 10 yaliyotolewa na Kiwanda cha Jielong Holdings (T) LTD kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya sekondari Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Kanunu akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko madawati 6 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Kanunu akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko madawati 6 kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Baptisti Kanunu, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ,viongozi na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati 6 yaliyotolewa na Kanisa la Baptisti kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya msingi Kizumbi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akiwataka wanafunzi katika shule ya msingi na sekondari Kizumbi kutunza viti, meza na madawati.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akiwataka wanafunzi katika shule ya msingi na sekondari Kizumbi kusoma kwa bidii na kuepuka utoro shuleni.
Wazazi, walimu na wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya akizungumza wakati zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Mkuu wa shule ya sekondari Kizumbi Marco Msangwa akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati ambapo alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 601, ilikuwa na upungufu wa madawati/viti na meza  460 na baada kupokea viti 40, meza 40 na madawati 10 sasa wana uhaba wa viti 19 na meza 19.
Afisa Mtendaji wa kata ya Kizumbi Joshua Masengwa akisoma taarifa ya kata  wakati wa zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Doris Dario akizungumzma wakati wa zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Wanafunzi wakifuatilia zoezi la makabidhiano ya viti,meza na madawati
Mwenyekiti wa CCM kata ya Kizumbi, Kudililwa Ndimila akizungumza wakati wa  makabidhiano ya meza,viti na madawati
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akipiga picha na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwaaga wanafunzi wa shule ya sekondari Kizumbi na kuwasihi wasome kwa bidii na kuepuka vishawishi.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post