Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dr. Luzila John akizungumza na mwandishi wa Malunde 1 blog ofisini kwake.
Na Josephine Charles - Malunde1 blog
Wito umetolewa kwa wananchi Mkoani
Shinyanga kuwa na utamaduni wa kupima afya ili kubaini
kama wana dalili za magonjwa yanayochangia ugonjwa wa figo.
Dk. Luzila ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani amesisitiza Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kupima Afya ili kubaini kama wana dalili za magonjwa yanayochangia kuwepo kwa maradhi ya Figo ikiwemo Kisukari,Presha,Tezi Dume na HIV/UKIMWI ili kudhibiti Ugonjwa huo kabla haujasababisha madhara mwilini.
Amefafanua zaidi kuwa Watu wazima kuanzia umri wa miaka 40,wanatakiwa kujiwekea utaratibu wa kupima afya mara kwa mara, ili kuweza kujikinga na magonjwa ya figo.
Aidha Kinga ya Ugonjwa sugu wa figo ni kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi, kula lishe bora na kamili, kunywa maji angalau lita 2.5 kwa siku, usafi wa mwili, kutokuvuta sigara au kunywa pombe kupita kiasi pamoja na kudhibiti shinikizo la juu la damu, kisukari na maambukizi ya mara kwa mara ya mfumo wa mkojo.
Kila Alhamisi ya wiki ya pili ya mwezi Machi Dunia huadhimisha siku ya figo duniani,ambayo ilianza kuadhimishwa rasmi Mwaka 2006 katika nchi 66 na baadae kuenea katika nchi zote duniani, lakini Nchini Tanzania siku hii ilianza kuadhimishwa Mwaka 2011.
Lengo
la kuadhimisha siku hii ni kufanya kampeni ya kidunia inayolenga kuongeza
ufahamu kwa watu juu ya umuhimu wa figo na kuwahamasisha kuchukua tahadhari ya
kujikinga dhidi ya maradhi ya figo na
matatizo mengine ya kiafya yanayohusiana na figo.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “ ISHI SALAMA NA UGONJWA WA FIGO”
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Luzila John.
Social Plugin