NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE
wa Viti Maalumu kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs)
Mh Neema Lugangira amesema Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) hapa nchini
zitampa ushirikiano mkubwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika
kutekeleza Dira na mipango yake ya maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Mh
Neema Lugangira ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa
kuchangia kwenye Maazimio Mawili; Kumuenzi Hayati Rais Magufuli na
Kumpongeza Mhe Rais Samia ambapo pia alisema kwamba wiki hii Asasi zaidi
ya 200 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar zimewasilisha tamko la pole na
salamu za Pongezi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassani ikiwemo Jukwaa la
Wanawake Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia (CSOs na NGOs) nao wametoa tamko
la pongezi kwa Rais.
Alisema
kwamba Sekta ya Asasi za Kiraia ina imani kubwa sana naye kwa sababu
anauzoefu mkubwa sana wa uongozi na mafanikio lukuki ambayo yatawezsha
kuleta tija kubwa kwa maendeleo ya Taifa letu la Tanzania
“Lakini
nitumie fursa hii kutaja maeneo machache: Mhe Rais Samia Suluhu Hassan
alianza ajira yake kwenye mwamvuli mashirika yasiyokwa ya kuserikali
linaloitwa ANGOZA (Association for Non Governmental Organisations in
Zanzibar) hivyo ni mwana Azaki mwezetu na ana uzoefu mkubwa ambao
utakuwa chachu kwetu”Alisema
Mbunge
Neema alisema Rais Samia anauzoefu mkubwa sana kwenye masuala ya
uwezeshwaji kiuchumi na kupitia uzoefu huo mwaka 2016 Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alimteua Rais Samia akiwa Makamu wa Rais
kuwa Mjumbe wa Jopo la Dunia kama Mwakilishi wa Afrika la kumshauri
namna bora ya kufanikisha Uwezeshwaji Wanawake Kiuchumi.
Alisema
la tatu ni kwamba miaka 25 iliyopita Rais Samia akiwa anatokea kwenye
NGOs alishiriki kwenye Mkutano wa Beijing uliokuwa unalenga kuleta
ukombozi wa usawa na kijinsia ikiwemo wanawake kwenye nafasi za uongozi
na maamuzi.
Aidha alisema
kupitia yeye kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Tanzania ameiwezesha
Tanzania kuweka historia ya kuwa sehemu ya Utekelezaji wa Maazimio ya
Beijing
Mbunge Neema
aliongezea kuwa akiwa kama mdau wa lishe wao wanatambua kuwa juhudi
kubwa ambazo Mhe Rais Samia ameweka katika kuhakikisha Serikali
inaboresha hali ya lishe hapa nchini.
Mbunge
huyo alisema vivyo hivyo wanatambua jitihadi kubwa za Makamu wa Rais
Mteule, Mhe Dkt Philip Mpango ameweka kwenye kuboresha hali ya lishe kwa
kuhakikisha kwamba Halmashauri zinatenga bajeti ya lishe kwa kulingana
na idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Mh
Naibu Spika napenda kuwasilisha ombi rasmi kwa Mhe Rais Samia Suluhu
Hassan la kukutana na Sekta ya Asasi za Kiraia ili nasi pia tuwe sehemu
ya mafanikio yake”,alisema Mbunge Neema
Lugangira
Social Plugin