MTOTO wa nyoka ni nyoka, msemo huo umetimia baada ya mtoto wa Wanamuziki matajiri duniani, Jay Z na Beyonce, Blue Ivy (9) kushinda tuzo yake ya kwanza ya Grammy ikimfanya kuwa mtoto wa pili mdogo kuwahi kushinda tuzo ya Grammy.
Baba na mama yake Blue Ivy, Beyonce na Jay Z wao wameshinda tuzo ya Music Bora (Best Music,) tuzo iliyotolewa mapema kabla matangazo rasmi kuanza.
The Record Academy imempongeza Blue Ivy huku wakimtag Blue Ivy ambaye kwà sasa hana twitter handle, akamtag katika akaunti za Beyonce na Wizkid.
Waliandika "Congrats Music Video winner "Brown skin girl @Beyonce #BlueIvy @Wizkid"
Akiwa ma umri wa miaka 9, Blue anakuwa moja ya watoto wadogo ambao wameshawahi kupata tuzo ya grammy.
Mwaka 2002 kundi la muziki la Peasall Sisters walishinda tuzo ya Album Bora kwenye soundtrack ya "O Brother, Where Art Thou?
Binti mdogo kabisa katika watoto hao wa kike, Leah akiwa na miaka 7, alirekodi na akiwa na miaka 8 akiwa na dada zake walishinda tuzo ya grammy.
Nyota njema huonekana asubuhi, Blue Ivy, hii ni nyota njema ambayo imeshaonekana asubuhi, daughter like mother, son like father.
Social Plugin