Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga kimeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani mwezi mzima (Machi) yanayofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania ( TGNP).
Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge kimeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo Alhamisi 11,2021 katika Kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambapo mgeni rasmi alikuwa Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ngazi ya jamii yaliyoandaliwa na TGNP kupitia Vituo vya taarifa na maarifa yamefadhiliwa na Kamesheni Kuu ya Watu wa Canada (Global Affairs Canada - GAC).
Awali wana kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge walitembelea na kukagua ujenzi wa Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Ukenyenge ambalo linajengwa kwa fedha za serikali shilingi milioni 80 kutokana na hamasa kubwa iliyofanywa na kituo hicho kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kupambana na mimba na ndoa za utotoni na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea kwenda shule.
Baada ya kutembelea jengo hilo la bweni,walifanya maandamano wakiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Ukenyenge kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wakiwa katika viwanja vya kijiji cha Negezi Wanakituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge walikabidhi Tanki la kuhifadhia maji katika zahanati ya Negezi lililotolewa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa ufadhili wa UNFPA.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Lagana wilayani Kishapu, Mhe. Janeth Sollo alisema akina mama wa Kata ya Ukenyenge wamejitambua,wanajihusisha na shughuliza ujasiriamali ili kujiinua kichumi akisisitiza kuwa wanawake wanaweza hata bila kuwezeshwa huku akiwataka wapendane, kuheshimiana na kujithamini kama wanawake wanaojitambua.
“Tunaushukuru Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuwawezesha wanawake kujitambua wilayani Kishapu. Mfano wanawake wengi katika kata hii wamepewa ardhi kuliko hata wanaume kutokana na kazi kubwa inayofanywa na mashirika katika kuwabadilisha kifikra wanawake na jamii kwa ujumla”,alisema Janeth.
“Tunaye mwanamke mahiri na shupavu sana, Fredina Said ambaye amekuwa mfano wa kuigwa katika kata hii katika masuala ya uongozi kwa sababu ni mama anayejitambua na ameweza na amewaunganisha wanawake wa Ukenyenge kuwa kitu kimoja”,alieleza Janeth.
Alisema endapo wanawake katika jamii watajitambua itakuwa rahisi sana kufikia dunia yenye usawa akibainisha kuwa mwanamke akikabidhiwa uongozi atajiheshimu kama kiongozi na atasimamia majukumu yake kikamilifu.
“Wanawake tukishirikiana,kuungana mkono na tukajiheshimu na kupendana, naamini kabisa tutakuwa wengi kujitokeza kugombea nafasi za uongozi. Tuanzie kwenye chaguzi za chama, tujitokeze kugombea uongozi na ifikapo mwaka 2025 tujitokeze kwa wingi kugombea”,alieleza.
Aidha aliwataka wazazi na walezi kusomesha watoto wote katika jamii na kuepuka kuwaacha nyuma watoto wa kike kwani mtoto wa kike ana haki ya kupata elimu kama alivyo mtoto wa kiume.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Anderson Mandia ambaye ni diwani wa kata ya Ukenyenge aliwashukuru wana vituo vya taarifa na maarifa na maarifa kwa harakati mbalimbali wanazofanya katika kuchochea maendeleo katika jamii na hasa kumfanya mwanamke kujitambua.
“Tunatakiwa kuanzia ngazi ya familia kuibua watoto wa kike ili kufikia dunia yenye usawa. Unakuta mtoto anapozaliwa tu unaona kabisa huyu atakuwa kiongozi hivyo ni vyema kuwaibua ili wawe viongozi",alisema.
Mandia alitumia fursa hiyo kuwaomba baadhi ya mama wa kambo kuacha kuwafanyia ukatili watoto hivyo wawapende, wawatunze huku akiwataka vijana kutunza mama zao kwa sababu upendo wa mama hauna kipimo.
Katika hatua nyingine alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma muhimu kama vile za afya na maji.
Kwa upande wake, Katibu wa Kituo cha taarifa na maarifa kata ya Ukenyenge, Fredina Saidi alisema wanaendelea kuwahamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ili kufikia dunia yenye usawa.
Fredina alisema ukatili wa kijinsia bado upo katika jamii akieleza kuwa hata kitendo cha wanawake kunyimwa nafasi za uongozi kutokana na mila na desturi kandamizi nao ni ukatili dhidi ya wanawake.
“Nashukuru kuona katika kata ya Ukenyenge wanawake sasa wameanza kupewa hati za kumiliki ardhi. Tunajitahidi kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye miradi ya maendeleo na serikali kutekeleza mahitaji ya wananchi, kwa kweli tunaishukuru sana serikali kwa kusikia kilio chetu cha muda mrefu cha maji ambapo sasa tunapata maji kutoka Ziwa Victoria, tumeletewa pia umeme na huduma za afya zinazidi kusogezwa”,aliongeza Fredina.
Akisoma risala ya kuhusu kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge, mwana kituo ,Anjelina Mahona alisema kituo hicho kiliundwa mwaka 2015 kikitokana na makundi mbalimbali ya wanawake ambao walijengewa uwezo na TGNP kuhusu namna ya kutatua changamoto mbalimbali za kijamii
Alisema hivi sasa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo bila kusukumwa na wanawake wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi ambapo sasa wapo viongozi wanawake kuanzia katika serikali za vijiji licha ya kuwepo kwa mila kandamizi zinazomfanya mwanamke akwame kufikia malengo yake.
Maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge yameenda sanjari na zoezi la kuwatambua wanawake vinara waliothubu kugombea nafasi za uongozi lakini wale walioonesha mabadiliko chanya dhidi ya mila na desturi zinazomkandamiza mwanamke na mtoto.
Kauli mbiu ya kidunia ya siku ya wanawake duniani mwaka 2021 inasema “Wanawake katika Uongozi: Fanikisha Usawa katika Dunia yenye COVID-19” Kitaifa, Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: “Wanawake Katika Uongozi: Chachu kufikia Dunia yenye Usawa” na upande wa TGNP ujumbe wake mkubwa ni “Badili Mitazamo kuleta Usawa” lengo kuu ni kuangazia wanawake katika uongozi na inaongozwa na msemo wa #ViongoziTuwaandaeSasa
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo (kulia) akicheza na akinama wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ukenyenge, Anderson Mandia akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge Peter Nestory akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge, Fredina Saidi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Katibu wa kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge, Fredina Saidi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge, Seleli Sendama akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Anjelina Mahona akisoma risala ya kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge, Fredina Saidi (kulia) akielezea kuhusu Tanki la Maji lililotolewa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) kwa ufadhili wa UNFPA kwa ajili ya zahanati ya Negezi kata ya Ukenyenge.
Kushoto mwenye nguo nyekundu ni Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo akimkabidhi Tanki na maji Muuguzi Mkunga Zanahati na Negezi kata ya Ukenyenge, Agnes William (katikati) wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Muonekano Tanki la Maji lililotolewa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) kwa ufadhili wa UNFPA kwa ajili ya zahanati ya Negezi kata ya Ukenyenge.
Muonekano wa Tanki la Maji lililotolewa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) kwa ufadhili wa UNFPA kwa ajili ya zahanati ya Negezi kata ya Ukenyenge.
Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo (kulia) akimkabidhi sukari na sabuni mama mwenye mtoto mwenye ulemavu wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Diwani wa Viti Maalumu kata ya Lagana Mhe. Janeth Sollo (kulia) akimkabidhi vifaa vya shule mtoto mwenye ulemavu Grace Joseph anayesoma darasa la saba katika shule ya msingi Kanawa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika kata ya Ukenyenge halmashauri ya wilaya ya Kishapu yaliyoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Ukenyenge Alhamisi Machi 11,2021.
Mtoto mwenye ulemavu Grace Joseph anayesoma darasa la saba katika shule ya msingi Kanawa kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu akiomba wadau wamsaidie kumnunulia baiskeli
Wana kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge wakitembelea na kukagua ujenzi wa Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Ukenyenge ambalo linajengwa kwa fedha za serikali shilingi milioni 80 kutokana na hamasa kubwa iliyofanywa na kituo hicho kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kupambana na mimba na ndoa za utotoni na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea kwenda shule.
Wana kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge wakitembelea na kukagua ujenzi wa Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Ukenyenge ambalo linajengwa kwa fedha za serikali shilingi milioni 80 kutokana na hamasa kubwa iliyofanywa na kituo hicho kinachosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kupambana na mimba na ndoa za utotoni na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea kwenda shule.
Muonekano wa Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Ukenyenge
Wanakituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge na walimu wakipiga picha ya kumbukumbu katika Bweni la wanafunzi wa kike katika shule ya Sekondari Ukenyenge
Mwana kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge akionesha mabango
Wana kituo cha taarifa na maarifa Ukenyenge wakionesha mabango
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge, Fredina Saidi akieleze namna walivyoshiriki kuhamasisha ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari Kanawa
Mkuu wa shule ya Sekondari Ukenyenge Juma Maganya akielezea kuhusu ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule hiyo.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza maandamano kutoka shuleni kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza maandamano kutoka shuleni kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakiandamana kutoka shuleni kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakiandamana kutoka shuleni kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakiandamana kutoka shuleni kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakiandamana kutoka shuleni kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakiandamana kutoka shuleni kuelekea katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi na Wana Kituo cha Taarifa na Maarifa Ukenyenge wakiwasili katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Akina mama wakicheza muziki katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ukenyenge wakicheza muziki kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wanawake na wanafunzi wakicheza muziki kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Ukenyenge, Naomi Benard akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge, Agripina Jastin Dyanze akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ukenyenge wakicheza mchezo wa Igizo kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Super Girls wakiimba shairi kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Mwakilishi wa Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Kishapu, Betila Martine akizungumza kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Afisa Mtendaji kata ya Ukenyenge, Leonora Alfred Kabuga akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Katibu wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino (TAS) wilaya ya Kishapu, Rashid Seif akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Mwakilishi wa Kikundi cha Wanawake Jeshi Kubwa, Mary Nyanda akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Mwakilishi wa shirika la REDESO, Godian Kabigumila akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wananchi wakicheza muziki kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yakiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin