Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amempongeza Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais mpya wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Dkt John Pombe Magufuli.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wake wa Twitter Rais Museveni amesema kuwa Uganda itafanya maombolezo ya siku 14 na kuongeza kuwa ''Roho yake ipumzike kwa amani''
Ujumbe huo wa Rais Museveni pia umeambatanishwa na taarifa ya awali ya rambi rambi aliyoitoa Rais Museveni kwa familia ya Hayati Magufuli pamoja na Watanzania kwa ujumla, iliyomsifu Magufuli kama rafiki wa Uganda, na kiongozi thabiti aliyepigania maendeleeo ya Watanzania na wanaafrika kwa ujumla:
Social Plugin