Mafundi wakiendelea na kazi kama wanavyoonekana kwa ajili ya kuuangisha Bomba kubwa la Maji |
Greda likiendelea na shughuli zake kama linavyoonekana |
Msimamizi wa Mradi
Mkubwa wa Kupeleka Maji Muheza kutoka eneo la kutibu maji la
Mowe,Mhandisi Salum Ngumbi kushoto akiteta jambo nMhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Peritach SB Limited
,Teobadi Nyalu katika anayefuatilia ni Afisa Uhusiano wa Tanga UWASA Devotha Mayala
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) Mhandisi Geofrey Hilly wa tatu kutoka kushoto akiwa na watumishi wa mamlaka hiyo wakiangalia namna shughluli zinazovyoendelea
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga
UWASA) imeunganisha bomba kubwa la maji ambalo litakuwa likitoa maji
kwenye mtambo wa kutibu maji wa Mowe uliopo eneo la Pande Jijini Tanga
mpaka eneo la Kilapula ambayo yatakuwa yakisukumwa kuelekea wilayani
Muheza ili kuondosha adha ya maji wilayani humo.
Akizungumza
wakati wa zoezi la uunganishaji wa Bomba hilo Afisa Uhusiano wa Mamlaka
la Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) Devotha Mayala
alisema maji hayo yatakapofika eneo la Kilapula yatakuwa yakisukumwa
kuelekea wilayani Muheza.
Devotha
alisema wanatekeleza shughuli hizo ili kuhakikisha maji yanapatikana
kwa wakati tofauti na awali ambapo maji yalikuwa yakipatikana kwa mgao
wa mara tatu kwa wiki tu, huku akiekeza pia wananchi wa Pongwe nao
watanufaika na mradi huo kutokana na kwamba hali ya huduma itaimarika na
maji yapatikana masa 24 na wao kama taasisi wataendelea kutekeleza
miradi mbalimbali kuhakikisha wanaondosha kero ya maji
Alisema
tokea walipokabidhiwa wilaya ya Muheza wananchi walikuwa wanapata maji
kwa asilimia 35 kwa mgao mara tatu kwa wiki na wanachofanya mwakia huu
kama taasisi ni kutekeleza miradi ya kuboresha huduma kwenye maeneo yao
mapya ya Muheza na wilaya ya Pangani.
“Kuna
mradi ambao unakwenda ukingoni wa kuboresha huduma ya maji Muheza
tulikwisha kujenga Tanki la Kuhifadhi Maji eneo la Kilapura na Pump
House ambapo tunaamini kwamba tatizo la maji Muheza litakuwa historia
“Alisema Afisa Uhusiano huyo.
Awali
akizungumza wakati wa utekelezaji wa shughuli hizo Msimamizi wa Mradi
Mkubwa wa Kupeleka Maji Muheza kutoka eneo la kutibu maji la
Mowe,Mhandisi Salum Ngumbi alisema kuwa kazi walionayo ni kuunganisha
toleo kubwa la bomba la milimita 300 ambayo ni hatua muhimu ya kupelekea
maji wilayani Muheza.
Mhandisi
Salum alisema litakapokamilika litawezesha wananchi wa wilaya ya Muheza
kupata maji masaa ya 24 na kuondoa mgao huku akieleza pia hali hiyo
itasaidia maeneo ya Muheza na Pongwe kupata maji masaa 24 na hivyo
wananchi kuondokana na adha ya kusaka huduma hiyo mbali .
Alisema
kwamba mradi huo ulianza mwezi May mwaka 2019 na unafadhiliwa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji na
una thamani ya shilingi ubilioni 2.6 ukiwa na lengo la kuwanufaisha
wananchi elfu 15000 wanaoishi mji wa muheza na wananchi 8000 wanaosihi
kwenye Vijiji vya Njiani kutokea Tanga kwenda Muheza.
“Kukamilika
kwa mradi huu utaongoza hali ya upatikanaji wa mji wa Muheza kutoka
asilimia 35 ya sasa mpaka kufikia 64 wananchi wa muheza watapata maji
siku saba za wiki na hivyo itawaondolea adha ambazo walikuwa wakikumbana
nazo awali”Alisema
Naye
kwa upande wake,Mhandisi wa Mradi kutoka Kampuni ya Peritach SB Limited
,Teobadi Nyalu alisema mradi huo walikabidhiwa May 30 mwaka 2019 wa
bomba lenye ukubwa wa milimita 300 na kulazma bomba kutoka Mowe hadi
Pongwe kilomita 8.2 ambapo kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za
utekelezaji wa mradi.
Alisema mpaka sasa wamekwisha kujenga chemba 20 na ufungaji wa vifaa mbalimbali ili kuwezesha wananchi kupata huduma.
Social Plugin