Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel Mzee Na Josephine Charles - Malunde1 blog
Jamii
imeaswa kuacha kutumia dawa za Kutibu Ugonjwa wa Malaria pasipo kufanya Vipimo
katika Vituo vya kutolea huduma za afya kwani kufanya hivyo kuna sababisha
usugu wa magonjwa mbalimbali katika mwili wa Binadamu.
Hayo
yamesemwa leo Alhamisi Machi 11, 2021 na Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga
Dk. Daniel Mzee wakati akizungumza katika Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa
na Radio Faraja Fm 91.3 Shinyanga kila
Jumatatu hadi Ijumaa.
Dk.
Mzee amesema nyumba bora nayo inachangia kupunguza tatizo la Malaria akieleza
kuwa pamoja na kwamba maisha ni magumu basi Jamii ijitahidi kutumia Chandarua
chenye Dawa,kuweka wavu dirishani ili Mbu wasipite pamoja na kuzingatia usafi
wa mazingira.
Amesema
Kauli mbiu ya malaria inasema “ZERO MALARIA INAANZA NA MIMI” hivyo kila mwananchi anapaswa kudhibiti vyanzo
vya uenezwaji wa Ugonjwa wa Malaria ikiwa ni pamoja na kufyeka nyasi,kufukia vidimbwi
vya maji kando ya nyumba anayoishi.
Kwa
Upande wa Takwimu ya Ugonjwa wa Malaria nchini Tanzania Dk. Mzee amesema
Tanzania ina kiwango cha asilimia 7.3% ya maambukizi ya Malaria wakati kwa Mkoa
wa Shinyanga kiwango cha maambukizi ni asilimia 6.1%.
Aidha
ameainisha viwango vya maambukizi ya Ugonjwa huo kwenye Halmshauri sita(6) za
Mkoa wa Shinyanga ambapo Halmshauri ya Ushetu ndiyo inayoongoza kwa kuwa na
maambukizi ya asilimia 11.1% ikifuatiwa
na Halmashauri ya Shinyanga ambayo ina asilimia 6.9%, Msalala asilimia 6.2%, Manispaa
ya Kahama ni asilimia 3.7% , Manispaa
ya Shinyanga ina asilimia 3.1 na Kishapu ina asilimia 2.9%.
Tazama picha hapa chini
Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel MzeeWatangazaji wa Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga Josephine Charles na Elisha Shambiti wakiwa Studio na Mratibu wa Malaria Mkoa Dr. Daniel Mzee.
Watangazaji wa Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga Josephine Charles na Elisha Shambiti wakiwa nje ya studio baada ya kipindi katika Picha ya Pamoja na Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel Mzee na Dereva wake.
Watangazaji wa Kipindi cha Mambo Leo kinachorushwa na Radio Faraja fm 91.3 Shinyanga Josephine Charles na Elisha Shambiti wakiwa nje ya studio baada ya kipindi katika Picha ya Pamoja na Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Dr. Daniel Mzee na Dereva wake.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com