WAFAHAMU VIONGOZI WA NCHI WALIOFARIKI DUNIA WAKIWA MADARAKANI BARANI AFRIKA


Mazishi ya aliyekuwa rais wa Ghana John Atta Mills
**
Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani. Hawa ni baadhi ya viongozi waliofariki dunia wakiwa madarakani barani Afrika.


Rais John Pombe Magufuli
John Pombe Magufuli

Kiongozi huyo wa Tanzania aliaga dunia tarehe 17 mwezi Machi 2021, miezi michache tu baada ya kuchaguliwa kwa awamu ya pili.

Kulingana na makamu wa rais Samia Hassan Suluhu, kiongozi huyo alifariki kutokana na mshtuko wa moyo baada ya kuugua tatizo hilo kwa zaidi ya miaka 10.

Kwengine mapema mwaka 2012, maelfu ya wananchi wa Ghana walihudhuria mazishi ya hayati rais, John Atta Mills, aliyefariki ghafla akiwa na umri wa miaka 68.

Rais Pierre Nkurunziza
Aliyekuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Rais Nkurunziza alifariki akiwa na umri wa miaka 55. Kulingana na Balozi Willy Nyamitwe , Nkurunziza alifariki kutokana na mshtuko wa Moyo , kinyume na uvumi uliokuwa ukienea .

Kulingana na ujumbe uliochapishwa katika Tmtandao wa Twitter Agosti 8 mwaka uliopita "Timu ya madaktari walishindwa kunusuru maisha yake baada ya kupata mshutuko wa moyo."

Rais Bingu wa Mutharika
Bingu wa Mutharika

Miezi minne kabla ya kifo cha Atta Mills, siku ya kitaifa ilitangazwa nchini Malawi kuwezesha maelfu ya watu kuhudhuria mazishi ya hayati rais Bingu wa Mutharika, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 78 kutokana na mshtuko wa moyo.


Mutharika wa Malawi alifariki dunia mwaka 2021 lakini ukosefu wa habari rasmi ulisababisha hali ya wasiwasi na uvumi nchini.


Lakini makamu wa rais Joyce Banda na Mutharika walizozana kufuatia mzozo wa kumrithi Mutharika 2010 ambapo alipigwa marufuku katika chama tawala cha Democratic party. (DPP).

Na mnamo mwezi Januari, rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha, alifariki katika hospitali ya kijeshi mjini paris baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 64.

Meles Zenawi wa Ethiopia
Meles Zenawi

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi alifariki akiwa na umri wa miaka 57 hospitalini ng'ambo, kulingana na serikali.

Serikali ya Ethiopia hatahivyo haikutoa maelezo lakini msemaji wa Muungano wa Ulaya baadaye aliambia waandishi kwamba Bwana Meles Zenawi alifariki mjini Brussels Ubelgiji.

Bwana Meles alikuwa hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa na kulikuwa na uvumi kuhusu afya yake wakati aliposhindwa kuhudhuria mkutano mjini Addis Ababa mwezi uliopita.

Makamu wake Hailemariam Desalegn alichukua uongozi hadi uchaguzi uliopoitishwa 2015.

Muammar Gaddafi
Muamar Gaddafi

Kiongozi wa zamani nchini Libya kanali Muammar Gaddafi aliuawa baada ya uvamizi katika Kijiji chake cha Sirte , maafisa wanasema.kaimu waziri mkuu Mahmoud Jibril alitangaza kifo chake na baadaye kusema kwamba kanali huyo aliuawa katika ufyatulianaji wa risasi kati ya wanajeshi wake na wapiganaji kutoka kwa mamlaka ya mpito.

Kanali Gaddafi aliondolewa mamlakani mwezi Agosti baada ya miaka 42 mamlakani.Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post