Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 60 kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Jamii imeitaka serikali kwa kushirikiana na Mashirika ya kiraia kuweka nguvu katika kutoa elimu ya Jinsia kwa wanaume wote ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo mila na desturi kandamizi.
Hayo yamesemwa jana Machi 25,2021 wakati wa mdahalo kwa wanaume wa kata ya Lunguya na Shilela katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Mkoani Shinyanga, uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Umoja la Idadi ya watu (UNFPA) kwa lengo la kuwafanya wanaume kupata nafasi ya kujadili, kutafakari na kupendekeza njia za kuondoa Ukatili wa kijinsia ikiwepo wao wenyewe kubadilisha mitazamo hasi juu ya wanawake.
Akizungumza, Mwezeshaji wa Mdahalo huo kutoka TGNP, Deogratius Temba, alisema kama wanaume watatumia vizuri nafasi yao vitendo vya Ukatili wa Kijinsia hasa unyanyasaji wa wanawake ikiwemo ndoa na mimba za utotoni vitapungua kabisa.
“Tukibadilisha mtazamo hasi juu ya wanawake, tukaona kuwa mtoto wa kike hawezi kuwa bidhaa ya kuuzwa ili tupate mahari, tukaondoka kwenye kutegemea uchumi wa ng’ombe kama njia ya kupata mali na kugeukia vyanzo vingine vya mapato tunaondoa kabisa tatizo la ndoa za utotoni”, alisema.
Washiriki walisema kwamba, suala la mahari linawaathiri vijana wengi kutokana na tatizo la ukosefu wa ajira pia.
Katika mdahalo huo uliowashirikisha vijana na wanaume kuanzia miaka 18 hadi 60 zaidi ya watu 300 kwa kata hizo mbili, suala la ulinzi wa kwa wasichana lilijadiliwa na kuazimia kutumia zaidi sheria ndogo ndogo za vijiji na jeshi la sungunsugu kulinda vijana wanaowarubuni wasichana wa shule.
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mshauri Jamii na Mtafiti kutoka TGNP, Catherine Mzurikwao akizungumza wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mkazi wa Shilela, Msigwa Pastor akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Mkazi wa Shilela Jumanne John akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mkazi wa Shilela Jumanne Masaga akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Mkazi wa Shilela Andrew Mayala akichangia hoja wakati wa Mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanaume kata ya Shilela Halmashauri ya wilaya ya Msalala
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mwezeshaji kutoka TGNP, Deogratius Temba akizungumza wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watu maarufu katika kata ya Lunguya kwa lengo la kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila na desturi zinazochangia ukatili wa kijinsia
Mganga wa Kienyeji Masanja Tabo akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mzee maarufu Helena Busobe akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Mzee Joseph Sonda akichangia hoja wakati wa mdahalo wa jamii kuhusu kutokomeza ukatili wa kijinsia katika kata ya Lunguya
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia:
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin